TANESCO mnatusababishia hasara kubwa kwa kukata na kurudisha umeme kila wakati

TANESCO mnatusababishia hasara kubwa kwa kukata na kurudisha umeme kila wakati

kasenene

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2008
Posts
1,632
Reaction score
2,413
Kichwa cha habari chahusika.

TANESCO toeni ratiba ya kata washa kata washa ifahamike kuliko jambo mnalotuanyia kwa sasa.

Hizi hasara za kutuunguzia vyombo vyetu sijui kama mtazibeba tukiamua kuwaburuza mahakamani. Siku hizi haieleweki lini mtu unakuwa na umeme. Halafu watu tunashindwa kupanga mikutano yetu (Teleconferences)
 
Hata TANROADS/TARURA nao wanasababisha uharibifu usio wa lazima wa vyombo vya moto, kuna maeneo wamakata kata vipande vya lami ili kuweka viraka, hadi sasa ni wiki ya pili na bado havijawekewa lami. Wanaruhusuje mkandarasi kufanya kazi kizembee ivooo bila ata kuweka alama
 
Kichwa cha habari chahusika....TANESCO toeni ratiba ya kata washa kata washa ifahamike kuliko jambo mnalotuanyia kwa sasa...Hizi hasara za kutuunguzia vyombo vyetu sijui kama mtazibeba tukiamua kuwaburuza mahakamani...siku hizi haieleweki lini mtu unakuwa na umeme...arafu watu tunashindwa kupanga mikutano yetu (Teleconferences)..
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Kichwa cha habari chahusika.

TANESCO toeni ratiba ya kata washa kata washa ifahamike kuliko jambo mnalotuanyia kwa sasa.

Hizi hasara za kutuunguzia vyombo vyetu sijui kama mtazibeba tukiamua kuwaburuza mahakamani. Siku hizi haieleweki lini mtu unakuwa na umeme. Halafu watu tunashindwa kupanga mikutano yetu (Teleconferences)
Wanazima na kuwasha kama beat ya singeli. Inafika hatua najiuliza hv kuna matengenezo ya switch kila siku?
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
Jaribu kuwa serious basi, watu wanalalamika vifaa vyao kuharibika kwa umeme mnaokata na kurudisha hovyo hovyo, jana eneo letu mlikuwa mnarudisha umeme mdogo ambao ulikuwa unarudi na kuzima kila baada ya dakika moja na hali hiyo ikaendelea kwa masaa matatu......
 
Ndio tunaomba taarifa kuwasikiliza na kuwapatia huduma,
 
Ndio tunaomba taarifa kuwasikiliza na kuwapatia huduma,
Kama hili swala linaathiri mamilioni ya watu, tuseme kwa kinondoni pekee............kila mmoja akituma taarifa humu tutaishia kujaza server, jitahidi kwenda na uhalisia.
 
Hivi Kunanchi Umem ewao Unaogopa Wingu la Mvua kama Tanzania yaani Hata kabla mvua kunyesha kawingu kidogo tu Kwaheri!

Na Niulize kwasasa kuna mkoa Umeme Unapatikana Masaa 24 yaani inatokea kuanzia Asubuhi mpaka Usiku haujakata?
 
Kama hili swala linaathiri mamilioni ya watu, tuseme kwa kinondoni pekee............kila mmoja akituma taarifa humu tutaishia kujaza server, jitahidi kwenda na uhalisia.
Swala la umeme au tatizo sio la watu wote bali linamuhusu mwenye tatizo hivyo hakuna majibu ya jumuiya kwa taarifa ya mtu mmoja mmoja,
 
Kama hili swala linaathiri mamilioni ya watu, tuseme kwa kinondoni pekee............kila mmoja akituma taarifa humu tutaishia kujaza server, jitahidi kwenda na uhalisia.
Nimeamua kununua solar, Tanesco kwa sasa ni Janga la Taifa
 
Swala la umeme au tatizo sio la watu wote bali linamuhusu mwenye tatizo hivyo hakuna majibu ya jumuiya kwa taarifa ya mtu mmoja mmoja,
TANESCO Nina Wiki 2 sasa Nipo Wilayani Urambo mkoa wa Tabora, Kuna shida gani Hii Wilaya yaani Umeme ni Hovyo hovyo

Unakatika Sana hakuna Utaratibu wowote. Kwasiku unakata na kurudi hata zaidi ya mara 10 iwe usiku,Mchana ndio hivyo
Shida nn kule
 
TANESCO Nina Wiki 2 sasa Nipo Wilayani Urambo mkoa wa Tabora
Kunashida gani Hii Wilaya yaani Umeme ni Hovyo hovyo
Unakatika Sana hakuna Utaratibu wowote
Kwasiku unakata na kurudi hata zaidi ya mara 10 iwe usiku,Mchana ndio hivyo
Shida nn kule
Eneo gani haswa na namba yako ya simu tafadhali
 
Nazungumzia Urambo Walayani mjimzima Hakuna cha Eneo wala nn
Namba yangu yann Kwani nashida Binafsi
Nimeuliza Wilaya nzima ya Urambo kuna shida au la
Mnaofisi kule ya Wilaya muulize mpaka saizi Umeshakata mara 3
na Haupo umeme
Hatuna tatizo la Wilaya Nzima Urambo ndio maana tuomba taarifa zako tukusikilize
 
Swala la umeme au tatizo sio la watu wote bali linamuhusu mwenye tatizo hivyo hakuna majibu ya jumuiya kwa taarifa ya mtu mmoja mmoja,
hii ndo athari ya haya mashirika kuajiriana kwa kujuana. Mtu anapewa kitendo cha 'customer care' lakini anakuwa na majibu mepesi mepesi tu kwa kukosa uelewa wa nini nafasi yake inahitaji.

Kwa akili yako wewe unaejibu maswali ya TANESCO nini maana ya jumuiya? kwa uelewa wangu ni kundi la watu linaloishi eneo moja. Sasa kama ushaambiwa eneo lote moja lilikatwa umeme halafu unajibu hakuna jibu la jumuiya unamaanisha muuliza swali kama anakaa Tabata basi umeme ukikatwa ama kurudishwa na hitilafu kwa eneo zima bado inabaki kuwa tatizo la mtu mmoja?

Mmekaririshwa jibu moja tu hapa JF kwa kila swali, nalo ni Jina, maeneo ulipo, namba ya simu. Lakini baada ya hapo hakuna la maana linalofanyika. TANESCO mnazingua sana. Na ni bora mkajitoa tu huku JF maana hakuna la maana mnalojibu zaidi ya kukera watu.
 
Nazungumzia Urambo Walayani mjimzima Hakuna cha Eneo wala nn
Namba yangu yann Kwani nashida Binafsi
Nimeuliza Wilaya nzima ya Urambo kuna shida au la
Mnaofisi kule ya Wilaya muulize mpaka saizi Umeshakata mara 3
na Haupo umeme
unapoteza muda wako tu ndugu yangu. Hakuna la maana utakalojibiwa hapa zaidi ya majibu ya jumla tu. Ukute huyo anaejibu swali kaweka miguu juu anachezea simu kusoma udaku instagram. Atakujibu kile anachojisikia ili masaa yake yatimie aende nyumbani kulala.
 
unapoteza muda wako tu ndugu yangu. Hakuna la maana utakalojibiwa hapa zaidi ya majibu ya jumla tu. Ukute huyo anaejibu swali kaweka miguu juu anachezea simu kusoma udaku instagram. Atakujibu kila anachojisikia ili masaa yake yatimie aende nyumbani kulala.
Hahaha Nimecheka Aisee
Umenena Ndugu wacha tutulie tu
 
Back
Top Bottom