TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Njia ya mtu muongo siku zote huwa ni fupi.

Anyway kuna watu wengi ndani ya JF walishatuonya miezi kadhaa nyuma inatafutwa sababu ya kupigwa deal.

Ngoja sasa tuambiwe gharama ya huo mtambo.

Ajabu zaidi logistic tu ya kununua huo mtambo na kuuleta hadi Tanzania udhani ni kama chini ya miezi mitatu; ina maana walijua mapema nchi itakuwa na giza la muda mrefu kweli kweli kuweza kufanya yao.

Only in Tanzania

Kuna kasyndicate kanatafuta pesa ya uchaguzi….👇🏼

 
TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.
Ripori pia iseme tumenunua au ndo tume kodi kama ile ya kina Richmond, Dowans au Aggreco!
 
Ijumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.

Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.

Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.

Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.

“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.

Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
View attachment 2437844
Ijumaa tarehe 2 Desemba wanafanya jitihada, siku mbili baadaye mtambo umewasili kutoka Marekani! Hawa jamaa wanatuona Watanzania mazuzu tusiojielewa.

Vv
 
Back
Top Bottom