TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Hizi jitihada za muda mfupi zimetugharimu sana kama Taifa, hasa kupitia hili shirika la Umeme, nitashangaa kama mwisho wa siku haitakuja kuwa kashfa, ni suala la muda tu.
Hizi ndizo zilimuondoa Lowasa kwenye uwaziri mkuu. Ila jamani hakika bongo kuna mchwa wasiokuwa na aibu. Hivi kipindi cha Dkt Magufuli mbona hapakuwa kabisa na dalili za kuagizia mitambo?????
 
R.I.P shujaa Magufuli
susp.png
 
Hilo ndo tatizo... nahisi kila mmoja ni kama anataka aandike historia yake...

Ule Mradi wa Kinyerezi kama ungekamilika, hivi sasa ingekuwa tuna umeme mwingi ambao hatuwezi hata "kuumaliza"

Na uzuri zaidi, hata lile Bwawa la Nyerere lingeweza kujengwa bila pressure hii iliyopo sasa!!!
Kwa sasa wanajikuta wanatumia hela nyingi kujenga vyanzo viwili kwa pamoja....
 
Hamna cha Dowans wala IPTL... ni ujinga tu wa viongozi...

Nchi tayari imeshaingia gharama ya zaidi ya Sh 1 TRILLION kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi.

Ambacho "kinatushinda" ni kujenga tu mitambo ya kuzalisha umeme pale Kinyerezi kwa sababu tayari gesi ipo!

Ukiangalia hiyo mipango yao utaona wazi ni ya kutegea mvua... kwamba mvua ikishanyesha, basi tatizo litapungua!
Watu wamegawana kuila Nchi
 
Ndio akili za watu wanaojinasibu wana-chadema hizo kwenye ili jukwaa wao mzaha kwenye kila kitu.

Sasa ndio nini ulicho post, si usome tu kama huna cha kuchangia.
Hilo Jambazi sio shujaa wala nini Aangamie kwenye moto wa milele.
 
Bwawa letu likiwa tayari hiyo mitambo itarudishwa ilipotoka?.
 
Wamalizie Plan ya JK ya kujenga Kinyerezi III na Kinyrerezi IV na sio kutegemea hii mipango ya zima kibatari....

Yaani wanachofanya ni kama wanatarajia baada ya muda mfupi mvua zitaanza kunyesha!
I am happy because you are around.
 
Ni watu wenye very simple minds, kazi yao kuropoka tu. Hawajui ata madeni iliyokuwa nayo TANESCO kwa suppliers wa gas were in trillions.
Kwa nini watu wengi mna act kama vile TANESCO hawana kipato. Sijawahi kuona seuemu yoyote taarifa ya mapato ya TANESCO kwa mwezi au mwaka. Kila siku tunasikia manunuzi, matatizo na madeni tu.

Sidhani kama kuna shirika lenye mapato makubwa kuzidi TANESCO. Tuanzie hapo.
 
Kwa nini watu wengi mna act kama vile TANESCO hawana kipato. Sijawahi kuona seuemu yoyote taarifa ya mapato ya TANESCO kwa mwezi au mwaka. Kila siku tunasikia manunuzi, matatizo na madeni tu.

Sidhani kama kuna shirika lenye mapato makubwa kuzidi TANESCO. Tuanzie hapo.
Financial Statements zao zipo kwenye website yao be it mara nyingi ni a year behind, mwaka huu awajaweka.

Kuna kila kitu unachotaka kuona about their finances and notes too on everything of your concern.

Last they made profits on EBIDTA and since 2017 there was an improvement on their finance. Hila kwa hawa I don’t think the same can be said.
 
Njia ya mtu muongo siku zote huwa ni fupi.

Anyway kuna watu wengi ndani ya JF walishatuonya miezi kadhaa nyuma inatafutwa sababu ya kupigwa deal.

Ngoja sasa tuambiwe gharama ya huo mtambo.

Ajabu zaidi logistic tu ya kununua huo mtambo na kuuleta hadi Tanzania udhani ni kama chini ya miezi mitatu; ina maana walijua mapema nchi itakuwa na giza la muda mrefu kweli kweli kuweza kufanya yao.

Only in Tanzania
Muongo Muongoze


Hawa Wanakwenda Kasi Kuhakikisha Wanatupiga Yaani US
 
Hivi naomba kuuliza huu umeme hautosh tz bara mbona zanzibar umeme hauzimwi hebu naomba kueleweshwa
Mafuta yalipnda bei huku bara zanzibar hayajapanda
Maji mgao zanzibar hkuna
Umeme tena mgao zanzbar hakuna au mi sielewi
 
Ijumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.

Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.

Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.

Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.

“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.

Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
View attachment 2437844
Hiyo kesi nyingine. Richmond mpya
 
Miaka miwili nyuma kulikuwa na umeme wa uhakika na lugha ilikuwa ya majigambo tunaweza miradi ya megawatts 2000+ na mfano juu.

Leo tumerudi na hadithi za megawatts 20.

R.I.P shujaa Magufuli
wanaombeza magufuli wana jehanamu yao spesho...
r.i.p magu
 
Tanzania na Afrika kwa ujumla tunahitaji kuwa na viongozi wanasayansi waliofanya kazi field kabla.
Ukoloni mamboleo bado upo, hasa hasa kupitia biashara za kimangungo unaotokana na ulimbukeni au ushawishi wa namna mbalimbali ikiwemo kifedha.
Kitu muhimu cha kujua ni kwamba, wazungu wanatutegemea waafrika, na wala siyo waafrika tunaowategemea wazungu.
Hata hivyo, kwa sababu ya fikra potofu zilizolaaniwa, viongozi na waamuzi wengi wanababaikia wazungu.
 
Back
Top Bottom