TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Ijumaa Desemba 2, 2022, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lilitoa taarifa ya jitihada za muda mfupi zilizokamilika pamoja na zinazoendelea kufanyika katika kukabiliana na upungutu wa umeme.

Leo Jumanne Desemba 6,2022, TANESCO imetoa ripoti kuwa tayari mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani siku ya Jumamosi Desemba 3, 2022.

Mtambo huo utafungwa katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Ubungo namba Ill.

Majaribio ya mitambo miwili katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I yanaendelea vizuri, na kwa sasa mitambo hiyo inaingiza jumla ya Megawati 65 za umeme katika Gridi ya Taifa.

Wamesema kuwa wanategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2022, mitambo hiyo itakuwa ikizalisha jumla ya Megawati 90.

“Bado tunaendelea na kazi za matengenezo ya mitambo miwili ya Ubungo namba Ill ambapo baada ya kukamilika mwishonl mwa Desemba 2022, itazalisha jumla ya Megawati 40 za umeme.

Kuhusu jitihada za kati Tanesco wamesema “Tunategemea mitambo mingine miwili kuanza kufanyakazi katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba I kuanzia mwezi Februari 2023 ili kuingiza Megawati 90 za umeme katika Gridi ya Taifa.
View attachment 2437844
Nasikia harufu ya Dowans!
 
Mambo ya masandarusi kama kazi !! Walisema mitambo ilikuwa haifanyiwi marekebisho kipindi kile !! Sasa ndio inafanyiwa matengenezo!! Na umeme ndiyo imekuwa shidaa !!
Tofautisha Maintenance na Extension....

Mwanzoni TANESCO walilaumiwa kutofanya MAINTENANCE ya Ubungo I na Ubungo II.

Hivi sasa taarifa inaonesha inafanyika Extension Pale Kinyerezi I, pia kuna mashine kwa ajili ya Ubungo III.

Unachofanya kwenye extension ni kuongeza idadi ya mashine kwenye existing plant.

Sema kiroja naona hicho cha kuagiza mashine inayoweza kuzalisha 20MW, na ndo maana nikasema mipango yao ni ya zima kibatari kwa matarajio kwamba mvua itanyesha!!

Sasa sijui gesi kutoka Songosongo haiwezi kuhimili mtambo mwingine wa kuzalisha MW nyingi zaidi ya hizo 20MW...
 
Huyo shujaa wako angejaza maji kwa mkojo? Kile kitendo cha kuacha mradi wa gas ambayo ilikuwa tayari kwenye stations ni kununulia tu mitambo na kuifunga ilikuwa wazo mfu kwasababu gas haina msimu kama maji.
Yani nchi iliendeshwa kwa kutumia ndoto za Nyerere za 70s kana kwamba dunia iko vile vile
Mwenda wazimu mwingine, hivi huwa mnasikiliza hata hayo maelezo ya TANESCO.

Toka wameanza kutumia hiyo gas kuzalishia umeme awajawahi lipa ata shilling kwa supplier thanks god ni TPDC, ilo deni serikali imelifuta.

TPDC nao wana deni la bomba la gas na uwekezaji wa mitambo; deni ambalo lilitakiwa kulipwa kwa kuwauzia gas TANESCO.

Madeni yote hayo yamerudi serikalini walalahoi wanapigwa tozo kuyahudumia na BoT wanaikausha vilevile.

Hiyo Gas awawezi lipia, halafu kila uchao mnapiga makelele gas this gas that.
 
Umeme wetu wategemea Mvua na Mwaka huu mvua zimekataa kabisa
Kwa ivyo solution ni kununua mtambo ambao ni less than 1% ya Nyerere Hydropower.

Au wangejikita kuumaliza mradi on time kama ilivyopangwa, badala ya kubadili matumizi ya hela za mradi na kuanza kumtungia uongo hayati.

Hadithi za kukauka kwa maji hizo ni sababu tu na sisi wasahaulifu enzi za Magufuli walituambia Mtera ikijaa inauwezo wa kutunza maji kwa miezi sita bila ya mvua. Nini kimebadilika siku hizi mvua ikikata mwezi na umeme hakuna.
 
hahahahaha naona 20MW gas turbine is in, halafu kuna pumbafu moja linakuja humu kutetea chama
 
Wamalizie Plan ya JK ya kujenga Kinyerezi III na Kinyrerezi IV na sio kutegemea hii mipango ya zima kibatari....

Yaani wanachofanya ni kama wanatarajia baada ya muda mfupi mvua zitaanza kunyesha!
'JK' wakati wake ulipita, sio rais wa nchi hii. Nchi haidaiwi kumalizia 'plan' zake.
 
Hili shirika uozo mtupu, huku kwetu wamekata umeme siku nzima kufika jioni unawaka unazima zaidi ya mara 4 sasa
 
Taarifa imejaa mauzauza na maneno ya kiulaghai. Mara upanuzi, mara matengenezo huku wanatupia tupia megawati na tarehe za kusadikika.

Cha ajabu nchi hii mvua ikianza kunyesha tu kuna uwezekano mkubwa umeme utakatika.
 
Huyo shujaa wako angejaza maji kwa mkojo? Kile kitendo cha kuacha mradi wa gas ambayo ilikuwa tayari kwenye stations ni kununulia tu mitambo na kuifunga ilikuwa wazo mfu kwasababu gas haina msimu kama maji.
Yani nchi iliendeshwa kwa kutumia ndoto za Nyerere za 70s kana kwamba dunia iko vile vile
Kwa bahati mbaya sana utakuwa huwa hata stori za vijiwe vya kahawa kuhusiana na gas na maji.

Ebu fuatilia ujue kuhusu Songas-PanAfrica-TPDC-Gasco-Tanesco na mnyororo unaendelea.

Halafu njoo hapa urudie hayo uliyoyasema
 
Ni watu wenye very simple minds, kazi yao kuropoka tu. Hawajui ata madeni iliyokuwa nayo TANESCO kwa suppliers wa gas were in trillions.
 
Hiyo Gas awawezi lipia, halafu kila uchao mnapiga makelele gas this gas that.
Mkuu, ongeza taarifa zaidi, andika kwa herufi kubwa.

Halafu tugeukie utaratibu wa manunuzi, ulifuatwa? Sheria zimevunjwa?

Mwisho, ka-turbine ka 20MW in 2022, kweli?

Wanahangaika kuongeza uwezo wa turbines zilizopo zitoke 35MW kwenda angalau 50MW, halafu wananunua 20MW?!!!!
 
Habari zipo wazi juzi tu waziri wa nishati na mkurugenzi wa TANESCO amerudia madeni waliyorudisha serikalini.
 
Back
Top Bottom