KERO TANESCO Mwanza, huku Nyamhongolo Stand, Ilemela tuna tatizo la umeme mdogo (low voltage)

KERO TANESCO Mwanza, huku Nyamhongolo Stand, Ilemela tuna tatizo la umeme mdogo (low voltage)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaiomba mamlaka husika hasa TANESCO kutatua tatizo la umeme mdogo (low voltage) katika eneo la Nyamhongolo Stand, Wilaya ya Ilemela, Mwanza.

Wananchi na wafanyabiashara wa eneo hili tunaendelea kupata hasara kubwa kutokana na umeme kuwa mdogo muda mwingi. Mashine za kazi haziwezi kufanya kazi vizuri, biashara zinakwama, na huduma zinakuwa ngumu.

Tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili eneo hili lipatiwe umeme wenye nguvu na wa uhakika kwa maendeleo ya wananchi na biashara.

Asanteni.
 
Pigeni Emergency TANESCO namba 180 au WhatsApp kwa 0748 550 000.
 
Habari, Ndugu Mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kujibu ujumbe wako kuhusu changamoto ya voltage ndogo (Low Voltage). Tulipata changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.

Tafadhali, tunaomba utufahamishe kama changamoto hiyo bado inaendelea au tayari imetatuliwa. Endapo bado hujapata msaada, tafadhali tujulishe ili tuweze kuifuatilia kwa kina na kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Pole sana kwa usumbufu uliotokea. Tunasubiri mrejesho wako ili tuweze kukusaidia zaidi.

Karibu sana. ^FL
 
Back
Top Bottom