TANESCO ndilo shirika linalochukiwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2023, hadi wahubiri wawaomba waumini kuwasamehe

Tatizo linalofanya kuchukiwa ni mwenendo wake ambapo kuna mashaka mashaka. Leo hii unakatiwa umeme usiku kucha unarudi saa tatu asubuhi halafu saa nane wanakata tena mpaka usiku saa tatu mbaya zaidi ni public holiday. Hakuna taarifa yoyote na cha kushangaza sehemu nyingine wao wanao ukirudi kwenu wale nao wanakula off. Mwanzo walisema maji mara wakaja mitambo haikufanyiwa service unashindwa ukamate kipi. Je Mh Kalimani waziri aliyekuwepo enzi zake alifanyaje kukawa hakuna mgao wa hovyo? Juzi Mhe Raisi kasema kuwa ikifika Januari,2024 mtambo wa bwawa la mwalimu Nyerere utaanza majaribio kwa mtambo mmoja yaani ni kama Tanesco wameambiwa sasa kata kweli kweli umeme. Nilitegemea kuona unafuu kumbe ndiyo balaa.Sasa watu wanakula sikukuu giza na joto hili unategemea watapendwa na utadhani huduma yenyewe ni ya bure.
 
CCM na TANESCO ndio taasisi zinazochukiwa kuliko zot.
 
TANESCO haina shida, shida ni Makamba na Chande ndiyo wamefilisi hili shirika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…