Tatizo la umeme lilianza January Makamba aliitisha kongamano kubwa la matajiri na viongozi mbalimbali kwa fedha nyingi za serikali.
Tatizo la TANESCO lilipanuka pale ambapo wanasiasa akiwemo Naibu WAZIRI Mkuu Biteko alipoanza kufanya siasa na kuacha kusema kweli kuhusu undani wa tatizo
Tatizo lilizidi kukuwa pale Mwenyenzi Mungu alipoleta mvua ambayo ilifuta kauli za ulaghai za wanasiasa kwamba mgawo unatokana na ukame.
Changamoto ilizidi kupanuka pale watendaji wa TANESCO walipokosa wakuwakemea au kuwawajibisha.
Kwa ujumla wamewakwaza wengi hasa ikizingatiwa ni shirika linalolipwa fedha za maslahi makubwa nchini.
Viongozi wa dini wameliona tatizo laTANESCO na kutuomba tuwasamehe ili Mwenyenzi Mungu afungue njia tupate watu sahihi kwenye sekta hii. Tumelitangaza shirika linalochukiwa ila pia tuamue sasa kusamehe may be 2024 Mwenyenzi Mungu atamwonyesha Mh. Rais safu mpya itakayosaidia kuondoa hizi fedhea.