TANESCO rudisheni token ama fedha za watu mlizochukua wakati wa tatizo la mtandao

TANESCO rudisheni token ama fedha za watu mlizochukua wakati wa tatizo la mtandao

Janja weed

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2020
Posts
3,000
Reaction score
5,606
Rudisheni Token ama fedha za watu mlizokata wakati mna tatizo la mfumo wa LUKU, ni muda sasa hela hamrudishi Token hamtoi, hamuoni kama huu ni wizi kama wizi mwingine?

Kwenye mitandao ya simu mtu akipata shida ya miamala ndani ya saa 24 hela zake zinarudi nyinyi mna tatizo gani , watu walinunua Token mara karibia 5 na hela zikakatwa kuna mtu alinunua umeme wa 20,000 mara tano akijaribu jaribu tu na zote zimekatwa mpaka leo hawajarudisha, wengine hadi laki mbili hadi leo kimya .

Hakuna anayejali wala kutoa ufafanuzi Si Waziri wala Nani , malalamiko yanaishia kwenye maji kama samaki.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

UTARATIBU WA KUREJESHA TOKEN

Juni 10, 2021,

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wananchi kuwa, kufuatia tatizo la manunuzi ya umeme kupitia mfumo wa LUKU Mei 17, 2021, TANESCO imeandaa utaratibu wa kuwarudishia umeme (token) wale wote walionunua na hawakupa namba za token au kutokuingia kwenye mita.

Ili kufanikisha zoezi hili unashauriwa kufika ofisi ya TANESCO iliyokaribu nawe au piga simu ukiwa na taarifa zifuatazo:-

1. Namba ya mita

2. Namba ya simu

3.Tarehe uliyonunua

4. Muda uliofanya manunuzi

5. Kiasi ulichonunua

6. Ujumbe unaopata ukiweka token.

Kwa wateja ambao wamewasilisha taarifa zao awali, tayari zinafanyiwa kazi.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliyojitokeza

Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Kirjaudu sisään Facebookiin

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
Huu ni uongo mtakatifu mambo yote hayo tumefanya lakini hakuna kilichorudishwa
 
Back
Top Bottom