888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 472
- 581
Wakuu wa JamiiForums, habari za muda huu.
Nimekuja hapa kuelezea machungu ya sisi wananchi wa Wilaya ya Simanjiro, hususan maeneo ya Terrat, na vijiji vyote vinavyopata umeme kupitia njia za Sinoni na Monduli.
Kiukweli hali ya umeme huku kwetu imekuwa ni kero isiyovumilika,Sijui kwa maeneo mengine TZ,, kwetu hapa imefika hatua, badala ya kusubiri umeme uwake, tunasubiri "SMS ya kuomba radhi" kutoka kwa TANESCO. Imekuwa ni ratiba sasa; kwa mfano wiki hii tarehe 25 umeme unakatika mara 3 kwa Siku , tarehe 27 asubuhi unakatika,tar.28 umekatika na maeneo ni yaleyale: kuanzia Kimotoro, Nyoriti, Lobosoit, Emboreet, mpaka huku Terrat, Losinyai, Oljoro na maeneo jirani.
Hivi TANESCO, hizi "Radhi" zenu ndio zitawasha mashine zetu za kusaga?
Tunashukuru kwa kutujulisha kuwa watalaamu wapo kazini, lakini kusema ukweli "Copy and Paste" ya jumbe za WhatsApp kila siku huku watu tunaharibikiwa na bidhaa kwenye majokofu haisaidii. Vinyozi hawawezi kufanya kazi, mafundi gereji wamesimama...
Inakuwaje njia hizi mbili (Sinoni na Monduli) zinapata "hitilafu" kila kukicha? Je, ni uchakavu wa miundombinu au ni uzembe wa kufanya matengenezo ya kudumu? Maana haiingii akilini njia hiyo hiyo inasumbua miaka nenda rudi bila ufumbuzi wa uhakika.
Tunawaomba viongozi wa TANESCO Mkoa wa Manyara na ngazi ya Taifa: Tumechoka kuwa wateja wa "Samahani", tunataka kuwa wateja wa "Umeme". Simanjiro tunachangia uchumi wa nchi hii kwa kiasi kikubwa, tunastahili huduma bora na siyo porojo za mitandaoni.
Wadau wenzangu wa huku Simanjiro na Arusha, hali ya huko kwenu ikoje? Hebu tupaze sauti labda wahusika wataamka.