TANESCO Simanjiro: Je, mnatupa Umeme au mnatulisha "Radhi" za WhatsApp?

TANESCO Simanjiro: Je, mnatupa Umeme au mnatulisha "Radhi" za WhatsApp?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
472
Reaction score
581
Wakuu wa JamiiForums, habari za muda huu.

Nimekuja hapa kuelezea machungu ya sisi wananchi wa Wilaya ya Simanjiro, hususan maeneo ya Terrat, na vijiji vyote vinavyopata umeme kupitia njia za Sinoni na Monduli.

Kiukweli hali ya umeme huku kwetu imekuwa ni kero isiyovumilika,Sijui kwa maeneo mengine TZ,, kwetu hapa imefika hatua, badala ya kusubiri umeme uwake, tunasubiri "SMS ya kuomba radhi" kutoka kwa TANESCO. Imekuwa ni ratiba sasa; kwa mfano wiki hii tarehe 25 umeme unakatika mara 3 kwa Siku , tarehe 27 asubuhi unakatika,tar.28 umekatika na maeneo ni yaleyale: kuanzia Kimotoro, Nyoriti, Lobosoit, Emboreet, mpaka huku Terrat, Losinyai, Oljoro na maeneo jirani.

Hivi TANESCO, hizi "Radhi" zenu ndio zitawasha mashine zetu za kusaga?
Tunashukuru kwa kutujulisha kuwa watalaamu wapo kazini, lakini kusema ukweli "Copy and Paste" ya jumbe za WhatsApp kila siku huku watu tunaharibikiwa na bidhaa kwenye majokofu haisaidii. Vinyozi hawawezi kufanya kazi, mafundi gereji wamesimama...

Inakuwaje njia hizi mbili (Sinoni na Monduli) zinapata "hitilafu" kila kukicha? Je, ni uchakavu wa miundombinu au ni uzembe wa kufanya matengenezo ya kudumu? Maana haiingii akilini njia hiyo hiyo inasumbua miaka nenda rudi bila ufumbuzi wa uhakika.

Tunawaomba viongozi wa TANESCO Mkoa wa Manyara na ngazi ya Taifa: Tumechoka kuwa wateja wa "Samahani", tunataka kuwa wateja wa "Umeme". Simanjiro tunachangia uchumi wa nchi hii kwa kiasi kikubwa, tunastahili huduma bora na siyo porojo za mitandaoni.

Wadau wenzangu wa huku Simanjiro na Arusha, hali ya huko kwenu ikoje? Hebu tupaze sauti labda wahusika wataamka.
 

Attachments

  • TANESCO LOGO.jpg
    TANESCO LOGO.jpg
    115.4 KB · Views: 57
Mkiambiwa muandamane hamtaki

So tulieni tu dawa iwaingie kama ulikataa kuandamana na kuwaona wanao Andamana Ni wajinga you have no right to blame,

Watu waliokuwa wame chagua kuandamana waliona kwamba hii njia mnayo tumia kulalamika mitandaoni imesha tumika sana lakini haijawahi kuzaa matunda that's why wakaamua kuandamana mkawaona wajinga so do you think unavyo lalamika huku serikali ndio itabadilika !? Serikali haiogopi malalamiko ya mitandaoni, ingekuwa inaogopa basi Nchi isingefika hapa tulipo ,
 
Tar 1 March umekatika kwanzia saa 2:30 Asb umerejea Saa 7:00 Mchn
 
Tar 2 March umekatika saa 10:23 jioni Hadi saa 1:40 usiku jumla saa 3+ hakukua na umeme
 
Tar 4 March umekatika saa 12:07 Asubuhi Hadi saa 3:38 Asubuhi jumla saa 3+ umekatika
 
Tarehe 4 March umekatika kwanzia saa 20:25 usiku Hadi tarehe 5 saa 13:49 Mchana
 
Tarehe 5 Machi umekatika saa 19:22 jioni ukarejea saa 20:19
 
Tarehe 7 umeme umekatika saa 16:19 jioni Hadi saa 19:21
 
Tarehe 8 Machi umekatika saa 00:12 ukarejea saa 08:32 Asubuhi
Ukakatika tena saa 13:46 ukarejea saa 15:16
 
Tarehe 9 Machi umekatika saa 01:47 Usiku ukarejea saa 07:58 Asubuhi
 
Tarehe 11 Machi umekatika saa 17:47 Hadi tarehe 12 saa 10:27 Asubuhi
Tarehe 12 ukakatika saa 14:13 ukarejea saa 14:56 , ukakatika saa 15:12 ukarejea saa 15:47
 
Back
Top Bottom