TANESCO Simiyu Bariadi imekuwa kero sana

TANESCO Simiyu Bariadi imekuwa kero sana

kamdudu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Posts
2,007
Reaction score
1,931
Habari Wanajukwaa wa JamiiForums ?

Natumai mko salaama.

Leo ni nina kero ya muda murefu sana kutokana na umeme wa huku Bariadi Mkoani Simiyu ambao umekua ukikatika na kurudi kila wakati kutwa nzima usiku kucha kama ka mchezo flani hivi.

Yaani umeme umaweza ukawaka kama dakika 30 hivi au lisaa limoja ukakata na ukarudi hapo hapo au baada kama ya sekunde 30 au dakika moja au ukakata ukipeleka mkono kwenye switch ili kuzima kwa kuepuka kuunguza vitu ile unaenda kugusa switch umeme huo ushawaka.

Hio umekua ni kama ka mchezo kwa miaka nenda rudi tulishaunguza vitu na tukaunguza tena na Malmaka ziko kimya kama vile hakuna kinachoendelea.

Tusaidieni kupaza sauti tujue nini mbaya maana imeshakua tatizo sugu Raia hata hatuelewi nini kinaendelea huko Tanesco.

Niwatakie jioni njema Nyote.
 
Ni wapi Tanesco siyo kero.
aise bora kama ni mgao mkaelewa moja na kama umeme umewaka uwake kama umekatika ukatike ila hii ya zima washa kutwa nzima usiku kucha ni zaidi ya kero
 
aise bora kama ni mgao mkaelewa moja na kama umeme umewaka uwake kama umekatika ukatike ila hii ya zima washa kutwa nzima usiku kucha ni zaidi ya kero
Usipoteze muda wako, tafuta solar backup.
 
Usipoteze muda wako, tafuta solar backup.
Tanzania hii umudu gharama ya kununua solar system ya kufua AC Volt 220 ili kuasha vifaa vyote vinavyotumia umeme ?

wewe naona unacheza kiduku
 
Back
Top Bottom