KUMALIZIKA KWA MKATABA WA UNUNUZI WA UMEME KATI YA TANESCO NA KAMPUNI YA UZALISHAJI UMEME KWA NJIA YA GESI ASILIA YA SONGAS
ljumaa 01 Novemba, 2024
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha umma kuhusu kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kutoka Kampuni ya uzalishaji umeme kwa njia ya Gesi asilia ya Songas. Mkataba huu umedumu kwa muda wa miaka ishirini (20) na umefikia ukomo wake jana tarehe 31 Oktoba 2024.
Pia soma:
Serikali: Mkataba wa Songas kumalizika Julai 2024
Pamoja na kufika ukomo wa mkataba huu Shirika linapenda kuwahakikisha wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni nzuri kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme ambapo kwa sasa uwezo wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya Gesi asilia na mitambo inayotumia maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini.
Hali hii imechangiwa na maendeleo mazuri ya Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere ambalo mpaka sasa jumla ya megawati 940 zimeungwa kwenye Gridi ya Taifa.
Pia soma:
Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024
Maamuzi ya Serikali kutokuendelea na mkataba huu ni kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya nchi. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO itaendelea kusimamia sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora, endelevu na ya uhakika ya umeme.
Pia soma:
Hii ndio hatari inayoweza kujitokeza baada ya mkataba wa Songas kumalizika
View attachment 3141013