TANESCO, Songas zamaliza Mkataba wa Uzalishaji Umeme. Serikali yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi

TANESCO, Songas zamaliza Mkataba wa Uzalishaji Umeme. Serikali yagoma kuendelea na mkataba kulinda maslahi ya nchi

"Sinunui umeme wako, na makubaliano yamekwisha duration time ni 20yrs, imekamilika, in peace,
That mean kuna phase 2, majadiliano itabidi yafanyike, #SONGAS aombe serekali inunue miundombinu, aidha songas itumie miundombinu hiyo kwa matumizi mengine, aidha apewe kazi ya kuuza gesi daresalam na mengineyo!

Biashara siyo mchezo wa hasira, tukae chini tukubaliane kununua kila kitu cha SONGAS ikiwemo mategemeo ya mapato waliyotarajia SONGAS kwa zaidi ya miaka mingine 20 kuanzia 2026 yaani 2050
 
Biashara siyo mchezo wa hasira, tukae chini tukubaliane kununua kila kitu cha SONGAS ikiwemo mategemeo ya mapato waliyotarajia SONGAS kwa zaidi ya miaka mingine 20 kuanzia 2026 yaani 2050
Remember this is not a breach, but the end of contract signed 20yrs ago!
 
Remember this is not a breach, but the end of contract signed 20yrs ago!
Plus that big thing - Implied Duties of Good Faith in Commercial Contracts :

Bates v Post Office[1]:
  1. There are no specific express terms preventing a duty of good faith being implied.
  2. The contract is long-term, with the contracting parties mutually intending a long-term relationship.
  3. The contract involves a high degree of communication, co-operation and predictable performance based on mutual trust, confidence, and expectations of loyalty.
  4. The contracting parties intend that their respective roles be performed with integrity, and with fidelity to their bargain.
  5. The contracting parties are committed to collaborating in the performance of the contract.
  6. The spirits and objectives of the venture may not be capable of expression exhaustively in a written contract.
  7. The contracting parties intend to place trust and confidence in one another (but of a different kind to that involved in fiduciary relationships).
  8. There may be a degree of significant investment /substantial financial commitment by one contracting party (or both) in the venture.
  9. The relationship may be exclusive.
 
Asante shujaa wetu kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa la Nyerere. Bila wewe kuanzisha huo mradi tungeendelea kupigwa mpaka tukomae. Sasa tunao ujasiri wa kusitisha mikataba isiyo na maslahi mapana kwa taifa. Rip JPM!
Mkataba umeisha au umesitishwa?
 
JPM aliyafanya haya akitimiza ilani ya CCM, mahaba yetu yanampa heshima kubwa huku tukisahau yeye alitimiza ilani ya Chama chake baada ya kukabidhiwa na kuagizwa aitimize.
Ilani bila uthubutu wa utekelezaji ni porojo tu kama porojo zingine. Kwani wakati tunasaini mikataba ya kipigaji enzi za akina Kikwete hapakuwa na ilani? Au ilani ndiyo ilielekeza tusaini mikataba ya kijinga isiyo na maslahi kwa nchi?
Mimi naona utendaji, wewe unaona ilani: hayo ni maono mawili tofauti!
 
Umeisha. Na kwa kuwa sasa tuna jnhpp, tuna ujasiri wa kuamua kurenew au kutokurenew!
Ku renew au kuto renew mkataba ni haki ya serikali, hivyo hilo si jambo linalohitaji ujasiri wowote.

Ungeongelea ujasiri kama serikali ingesitisha mkataba ambao haujaisha.

Sasa serikali ambayo imesubiri mpaka mkataba uishe ina ujasiri gani?
 
KUMALIZIKA KWA MKATABA WA UNUNUZI WA UMEME KATI YA TANESCO NA KAMPUNI YA UZALISHAJI UMEME KWA NJIA YA GESI ASILIA YA SONGAS​

ljumaa 01 Novemba, 2024

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha umma kuhusu kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kutoka Kampuni ya uzalishaji umeme kwa njia ya Gesi asilia ya Songas. Mkataba huu umedumu kwa muda wa miaka ishirini (20) na umefikia ukomo wake jana tarehe 31 Oktoba 2024.

Pia soma: Serikali: Mkataba wa Songas kumalizika Julai 2024

Pamoja na kufika ukomo wa mkataba huu Shirika linapenda kuwahakikisha wateja wake kuwa hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni nzuri kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme ambapo kwa sasa uwezo wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya Gesi asilia na mitambo inayotumia maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini.

Hali hii imechangiwa na maendeleo mazuri ya Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere ambalo mpaka sasa jumla ya megawati 940 zimeungwa kwenye Gridi ya Taifa.

Pia soma: Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024

Maamuzi ya Serikali kutokuendelea na mkataba huu ni kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya nchi. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO itaendelea kusimamia sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora, endelevu na ya uhakika ya umeme.

Pia soma: Hii ndio hatari inayoweza kujitokeza baada ya mkataba wa Songas kumalizika

View attachment 3141013
msizuge nyie semeni tu amepewa ROSTAM
 
Ku renew au kuto renew mkataba ni haki ya serikali, hivyo hilo si jambo linalohitaji ujasiri wowote.

Ungeongelea ujasiri kama serikali ingesitisha mkataba ambao haujaisha.

Sasa serikali ambayo imesubiri mpaka mkataba uishe ina ujasiri gani?
Kuheshimu mkataba pia ni ujasiri
 
Kuheshimu mkataba pia ni ujasiri
That is beside the point.

Mimi sitetei kuvunja mikataba.

Ninachosema hapa ni kwamba, suala la serikali kutoendeleza mkataba ulioisha ni suala la haki ya serikali tu, si suala la ujasiri.
 
..maamuzi magumu, au anataka kuleta kampuni ya maswahiba zake?

..hukusikia Abduli ana kampuni ya kwenye briefcase inayojihusisha na masuala ya energy?
Hata BANDARI MKATABA WA T.IC.S ILIISHA,GHAFLA AKAJA MWEKEZAJI MWINGINE "DP WORLD"
TUNAVIZIWA,UTASIKIA TUMEINGIA MKATABA WA MUDA MFUPI .
TUNASHAURI,SERIKALI INUNUE MTAMBO(imilikiwe na Serikali) TUMALIZANE NA SONGAS,Tuwe na meme wa bei nafuu.Vinginevyo tutasahulishwa!,wapenda pesa walete tena mikataba yenye kuumiza TANESCO.
 
Kama NHHEP imekamilika kwanini iwashwe mitambo michache.
 
Ni wakati sasa wa Tanesco kuwekeza sana kwenye gas plants baada ya kuachana na wazungu. Haya mapesa walikuwa wanatumia kulipa Songas na wenzao, yaelekezwe kwenye kujenga gas plants za kwetu. Hili bwawa tunatamba sasa hivi, baada ya miaka 30 tutarudi hapa hapa kama hatutatumia fursa vizuri
 
Back
Top Bottom