TANESCO tuambieni nini kinaendelea huko Mbeya maana umeme kukatika imezidi sasa

Ahsante kwa taarifa

Tunawajulisha kuwa kuna kazi inaendelea kwenye kituo chetu hivyo mara baada ya kumaliza kazi hali ya umeme itatengemaa kama hapo awali

Kituo kipi maana hili tatizo liko nchi nzima, tena hili tatizo lilianza wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2020. Kadiri siku zinavyokwenda tatizo linazidi kuwa kubwa, na sasa ni karibu nchi nzima umeme unakatika hovyo, tena sio kukatika tu, bali unakatika muda mrefu kwa siku. Sasa unaposema kirahisi kuwa kuna kazi inaendelea bila ufafanuzi ni kama unatuingiza mjini.
 
Kwetu tulishazoea mgao sasa.

Ngoja tukatafute solar tuendelee na maisha yetu.
 
mkuu sio mbeya tuu, hili tatizo sasa ni karibia mikoa yote, hawa jamaa wanarudisha sana juhudi nyuma, imefkia kipindi sasa serikali iwawajibishe kuanzia ngazi za juu mpaka chini, ilikusudi juhudi ziendelee kusonga mbele kwa mbele.
Unadhani serikali hawajui kinachoendelea? Tatizo lote linaanzia huko huko serikalini.
 
Unadhani serikali hawajui kinachoendelea? Tatizo lote linaanzia huko huko serikalini.
Wewe jamaa mbona unapenda kulaumu sana? Umeambiwa kunahitilafu na ukarabati unafanyika bado unataka kulaumu serikali.

Au wizi wa kura unahusika?
 
Wewe jamaa mbona unapenda kulaumu sana? Umeambiwa kunahitifu na ukarabati unafanyika bado unataka kulaumu serikali.

Au wizi wa kura unahusika?

Ww ni msemaji wa TANESCO? Amesema kuna kituo wanafanya marekebisho, nimemwambia ni kituo gani, maana hili tatizo liko nchi nzima na lina zaidi ya miezi mitano sasa, na linaendelea kuwa kubwa. Aidha ujibu ww ni kituo gani mpaka kuna tatizo nchi nzima tena kwa muda mrefu?
 
Dawa yake kuwe na mashirika shindani ya kuuza Umeme.!
Dawa yake kumtumbua mkurugenzi na team yake. Leta vijana under fourty ambao tunao wengi tu na hawahitaji Viieite kufanya kazi.
Wape IST au Bajaj wata deliver
 
Na hapa Dar imekuaje?. Maana toka jana Kimara umeme unasumbua
Mitaa ya Banana ,Goms kuna mgao wa kimya kimya?
Umeme unakata kwanzia SAA 6 mchana unarudi SAA tano usiku hii Siku ya tatu sasa
 
,
Je kama ni kituo unganishi cha grid ya taifa? Kuhusu miezi mitano sio kweli.Mimi ninazunguka hii nchi sana. Jana Igunga kulikuwa hamna umeme.
 
,

Je kama ni kituo unganishi cha grid ya taifa? Kuhusu miezi mitano sio kweli.Mimi ninazunguka hii nchi sana. Jana Igunga kulikuwa hamna umeme.
Huku kwetu hii Siku ya tatu umeme unakata saa 6 au 5 mchana unarudi 6 au 5 usiku na hakuna taarifa yoyote...

Wanakwamisha sana kazi za watu....hapa ninavyozungumza wamekata tayari
 
,

Je kama ni kituo unganishi cha grid ya taifa? Kuhusu miezi mitano sio kweli.Mimi ninazunguka hii nchi sana. Jana Igunga kulikuwa hamna umeme.

Umevamia mada yangu kizalendo ndio maana hujaelewa nimesema nini. Nimesema hivi, hili tatizo la kukatika kwa umeme limeanza rasmi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, kadiri siku zinavyokwenda ndio tatizo linazidi kuwa kubwa. Na kuna uzi nilichangia hapa kabla ya uchaguzi mkuu kuwa kuna tatizo la kukatika kwa umeme, Ila viongozi wako kimya ili Ile hali isiwatilie doa kwenye uchaguzi. Ndio maana umeona hiyo verified user ya TANESCO imeishia kutoa maelezo hafifu kwakuwa anajua kila kitu kinachoendelea. Ila kwakuwa ww unajifanya kuitetea serikali ndio maana umeivaa hii mada kichwa kichwa ukiwa huna jipya.
 
Ahaaaa . Oktoba mwaka jana umeme haukukatika kama mwaka huu. Mimi sitetei wala sio muimba mapambio.
 
Subiri stegolazi goji iishe...mi7 tena.
 
Ahaaaa . Oktoba mwaka jana umeme haukukatika kama mwaka huu. Mimi sitetei wala sio muimba mapambio.
Jifunze kusoma na kuelewa boss, nimesema tatizo hili la kukatika lilianza miezi zaidi ya mitano iliyopita, ila kadiri muda unavyokwenda linazidi kuongezeka. Nini huelewi hapo?
 
Jifunze kusoma na kuelewa boss, nimesema tatizo hili la kukatika lilianza miezi zaidi ya mitano iliyopita, ila kadiri muda unavyokwenda linazidi kuongezeka. Nini huelewi hapo?
Acha dharau,nijifunze kusoma?
Miezi mitano iliyopita ulisikia malalamiko nchi nzima?

Utetezi sio kusema kweli!
 
Acha dharau,nijifunze kusoma?
Miezi mitano iliyopita ulisikia malalamiko nchi nzima?

Utetezi sio kusema kweli!
Duuh majibu yako yanafikilisha uchakataji wako wa data mzee baba.
 
Acha dharau,nijifunze kusoma?
Miezi mitano iliyopita ulisikia malalamiko nchi nzima?

Utetezi sio kusema kweli!

Kwa taarifa yako kuna uzi uliojadili suala la kukatika kwa umeme kwenye mwezi wa tisa au kumi humu jukwaani. Kwani sasa hivi unapimaje malalamiko ya nchi nzima ambapo huko nyuma hakuweza?
 
Kwa taarifa yako kuna uzi uliojadili suala la kukatika kwa umeme kwenye mwezi wa tisa au kumi humu jukwaani. Kwani sasa hivi unapimaje malalamiko ya nchi nzima ambapo huko nyuma hakuweza?
Malamiko toka sehemu mbalimbali za nchi yanakupa picha gani? Tumian ubongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…