TANESCO tuambieni nini kinaendelea huko Mbeya maana umeme kukatika imezidi sasa

TANESCO tuambieni nini kinaendelea huko Mbeya maana umeme kukatika imezidi sasa

Yaani kama unajibu hoja kirahisi hivi ni bora ungekaa kimya tu
Hauwezi kusema"hilo tumelitolea taarifa leo kupitia clouds fm kipindi cha asubuhi"
Are you serious?
Ni wangapi wamekaa na kuisikiliza hiyo clouds fm?
Na tatizo limeikumba nchi karibu yote

Au hiyo taarifa mmewapa wanaosikiliza clouds redio
Sie wa vituo vingine haituhusu
Taarifa kwa umma haichagui chombo cha habari
Nyie Tanesco maisha ya watanzania yapo mikononi mwenu
Bila umeme hamna ajira
Bila umeme hamna mapato

Bila umeme hamna wawekezaji
Leteni masikhara
Namshangaa waziri na naibu wake wamekaa tu ofisini wanatoa matamko
"Tuna umeme wa kutosha..... Bla...bla...blaaa nyingi badala ya kuingia site kuona tatizo ni nini
Hawa jamaa hawajawahi kuwa serious. Tatizo kubwa linaloathiri uchumi na maisha ya watu kwa ujumla halafu majibu mepesi tu. Yaani utafikiri huo umeme wanatuwagia bure tu. Hopeless kabisa!!
 
Sinza ndo kama hivi muda huu, tushazoea yani ni daily dose
JPEG_20210301_190706_8536642501435575473.jpg
 
Ahsante kwa taarifa

Tunawajulisha kuwa kuna kazi inaendelea kwenye kituo chetu hivyo mara baada ya kumaliza kazi hali ya umeme itatengemaa kama hapo awali
Na Singida vijijin shida nn Mkuu ? maana umeme tunapata kwa manati Sana
 
Ahsante kwa taarifa

Tunawajulisha kuwa kuna kazi inaendelea kwenye kituo chetu hivyo mara baada ya kumaliza kazi hali ya umeme itatengemaa kama hapo awali
Asante kwa taarifa ila ni vyema tungejulishwa hiyo kazi inatarajia kuisha lini.
 
Ni takribani miezi kadhaa sasa, Mkoa wa Mbeya imekuwa kero, Umeme Unakatika Zaidi ya mara 4 kwa Siku.

Na hili tatizo lipo zaidi ya Miezi 3 hivi.

Tunaambiwa Bwawa la Mtera Maji yamejaa mpaka wanayafungulia yatoke lakini Umeme katika Siku nzima unawaka si zaidi ya Saa 6 hivi.

Tafadhalini acheni Siasa tunaomba Majibu maana hata hamtoi Taarifa yeyote.

Nawasilisaha.
Kweli imekua too much
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MACHI 01, 2021

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME KWA GESI VYA SONGAS NA UBUNGO II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa tunaendelea kufanya matengenezo ya miundombinu ya Umeme katika vituo vya kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Songas na Ubungo II.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya Umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mitambo inatengemaa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadili kazi ya matengenezo inavyoendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanesco_official_page

Barua pepe: [email protected],

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu

Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Kumbe mnazo accounts kwenye social medias karibu zote, inakuaje mnashindwa kutoa taarifa ili zifikie wananchi wengi.
Msirudie tena kutangaza clouds peke yake maana hamjatununulia radio na hatujui ni wakati gani mtatangaza radioni.

Hii taarifa pia haijakamilika. Ni lini mnatarajia kumaliza marekebisho? Miezi 6, miaka 2. Elezeni vizuri tuelewe.
 
Ahsante kwa taarifa

Tunawajulisha kuwa kuna kazi inaendelea kwenye kituo chetu hivyo mara baada ya kumaliza kazi hali ya umeme itatengemaa kama hapo awali
Hamjawah kuwa na awali njema nyie
 
Back
Top Bottom