TANESCO wakanusha taarifa ya MWAUWASA kuhusu upungufu wa maji Mwanza

TANESCO wakanusha taarifa ya MWAUWASA kuhusu upungufu wa maji Mwanza

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekanusha madai yaliyotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwamba changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mwanza imesababishwa na kukosekana au kuyumba kwa huduma ya umeme kwenye mitambo ya uzalishaji maji.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja ya TANESCO Makao Makuu, shirika hilo limesema taarifa ya MWAUWASA ya Juni 9, 2026 si sahihi kwani hakukuwa na hitilafu yoyote ya umeme iliyoweza kuathiri uzalishaji wa maji katika kipindi husika.

TANESCO imeeleza kuwa si mara ya kwanza kwa MWAUWASA kuhusisha changamoto za maji na huduma ya umeme ikirejea madai kama hayo yalitolewa pia mwezi Septemba 2025.

"Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa hitilafu zilizokuwa zikijitokeza zilisababishwa na changamoto za ndani za mitambo ya uzalishaji maji ya MWAUWASA na si hitilafu za huduma ya umeme kutoka TANESCO,".

Tayari hiyo imeongeza kuwa "ilibainika kuwa baadhi ya mitambo ilizimika wakati huduma ya umeme ikiendelea kupatikana katika viwango vya kawaida vya voltage vinavyokubalika kitaalamu, jambo lililoonesha kuwa chanzo cha changamoto hizo kilikuwa ndani ya mfumo wa mitambo ya MWAUWASA,".

Hata hivyo shirika hilo limeeleza kuwa baadhi ya mapendekezo hayo muhimu bado hayajatekelezwa, huku likisisitiza kuwa hakuna ushahidi unaoonesha kuwa huduma ya umeme ndiyo iliyosababisha changamoto ya uzalishaji na usambazaji wa maji iliyolalamikiwa.

"Si sahihi kuhusisha au kulaumu taasisi nyingine zisizohusika wakati wa changamoto kwani hatua hiyo inaweza kupotosha umma na kuathiri taswira chanya ya taasisi zingine," imesema taarifa hiyo

Taarifa ya MWAUWASA
20260614_162745.jpg


Taarofa ya TANESCO
20260614_162746.jpg


Pia soma: MWAUWASA: Kukosekana kwa huduma Uzalishaji na Usambazaji wa Maji Mwanza imetokana na hitilafu ya umeme
 
haya mashirika yana mamilioni ya wateja wanaweza kuwapata bila hata kujitangaza na ambao wako tayari kulipa chochote ili wapate huduma, lakini huduma za hovyo na hasara kila siku, hawa watu ni zaidi ya takataka 👎
 
Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa hitilafu zilizokuwa zikijitokeza zilisababishwa na changamoto za ndani za mitambo ya uzalishaji maji ya MWAUWASA na si hitilafu za huduma ya umeme kutoka TANESCO,".
Nawapongeza TANESCO zigo la lawana wasipewe wao kila mmoja abebe msalaba wake mwenyewe. MWAUWASA wawajibike kwa makosa au uzembe wao
 
Nchi inaendeshwa kama ghetto la masela.
Mifumo haisomani.
Naomba weka Heshima kwz kwa Ghetto la Masela! Lipo organized! Straight forward!
SSupportive kwa wana!
 
Back
Top Bottom