Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Yaani kama ni mradi basi watu wa TANESCO wanajua kutia hasara. Nitagusia mambo matatu
Kwanza kabisa hawa jamaa wakibakiza vifaa kwenye kazi zao sioni wakivifuata wala kuvitunza. Nyaya kila sehemu wameacha, machuma chuma kibao wanayatelekeza ovyo
Pili hawa vijana wa TANESCO wa siku hizi naona ni tofauti kabisa na wale wa zamani katika kazi. Haiwezekani kila wanapofanya kazi mavifaa kibao yabaki mfano tuchukulie nyumba x kumebaki liwaya hilo halafu mkabala nyumba y nayo kunabaki pande lingine la waya. Haya ni matumizi ya fujo
Tatu naomba kuelimishwa hivi zile sheria za kuvutiwa umeme mpaka ununue bomba zimefutwaga? Maana siku hizi waya za umeme tunazishika na mikono kabisa zilivyo chini (sitanii). Siku hizi naona umeme ni zigizaga tu hivi kuna mpangilio maalum kweli unazingatiwa?
KItu kingine ambacho niliwahi kusema humu na ndiyo kinachowagharimu kwa namna fulani, hawa jamaa huwa wanajidai hawana sheria wakitaka kufanya kazi zao hawana kumuona nani wala nani matokeo yake kuna sehemu mtu wao alipanga chumba (walikuwa wamepiga kambi ya muda huko) akaacha makorokoro chumba kizima na hakurudi. Mwenye nyumba kakaa na vitu vile zaidi ya mwaka ikabidi akatolee taarifa ofisini.
Yote kwa yote, TANESCO fuatilieni kwani vijana wenu wanahujumu shirika. Haiwezekani rola zima la waya (sijui linaitwaje jina lake halisi) linaachwa mpaka mchwa wanakula mbao zote unabaki waya tu, Machuma watoto wanaokota wanachezea tu.