Nalileta hili kwenu kwa sababu nimeona madhara mengi kwa wananchi.
TANESCO, mnatakiwa mkishapima eneo, hasa kwenye miradi mikubwa ya nguzo za chuma, muweke alama zenu za mawe (bicon). Sababu ni kwamba maeneo ya mwisho wa mipaka yenu huleta mizozo mingi na wananchi.
Hata kama mradi wa kujenga nguzo bado haujaanza, mnatakiwa muwe tayari mmeweka Bicon zenu. Haya ndio madhara yanayotokea kwa wananchi wanapolazimika kuhisi mipaka yenu:
1. Mwananchi anaepakana na mradi huu, pindi anapojenga fensi, hujikuta akijidhulumu hatua mbili au tatu wakati mnapokuja kuweka Bicon zenu baada ya makazi kujaa.
2. Mwananchi hujikuta anapata hasara ya kubomoa nyumba au fensi baada ya kujikuta amejiingiza hatua moja au mbili ndani ya eneo la TANESCO.
Kuweka alama ni jambo bora linalosaidia kuokoa mali, fedha, na maisha ya watu. Kama ilivyo kwa alama za barabarani ambazo humsaidia dereva kuendesha gari kwa usalama
By mwanakijiji-Mkonze_Dodoma