Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Status
Not open for further replies.
Kama habari hii ya kweli, basi jitihada za Magu zinastahili kupongezwa sana, maana ufisadi mkubwa uko kwenye hili limkataba, sijui nani yuko nyuma yake ,maana historia ya IPTL ukiligusa tu wew ndo unakwisha .
 
Hapo JPM amecheza vizuri sana, sasa ni kwamba fedha zote ambazo walitakiwa kulipwa hao IPTL zimesitishwa nadhani wanasubiri rufaa iliyokatwa na TANESCO, kama TANESCO wakishindwa kesi basi fedha hizo walipwe Standard charted tu.

huo mtambo wa IPTL utaifishwe tu, nadhani na IPTL wanaweza kuacha kutuuzia UMEME, hapo ndo patamu ili mkataba uvunjwe tu
Ushawahi kusikia tumeshinda kesi mimi sikumbuki nifahamisheni
 
yule mtaalam mzee wa makabrasha iwe bojo yuko wapi siku hizi haonekani.ndo mwanzilishi wa yote haya akishirikiana na viongozi wetu enzi hizo wenye njaa ya rushwa.
mara ya mwisho mzeehuyu alionekana chijijini bukoba akinywa heineken na wazee
 
Mambo mengine ni burudani kweli
Mtu umejinyea kwa uchafu mwenyewe, halafu unapojisafisha unataka usifiwe.
 
Kwa hili la IPTL lina siri kubwa kwa kwa viongozi waliomtangulia Rais wa awamu ya tano.Tuliona jinsi management ya TANESCO ilivyosambaratishwa na awamu ya tatu na wafanyakazi kurudi kazini kwa kusimamiwa na polisi na hapo ndipo shirika likaingia katika matatizo hadi leo.Kwani watanzania tunasononeshwa na makampuni ya kufua umeme hasa katika capacity charges maana kipengele hichi ni wizi Mungu ampe ujasiri Rais wa awamu ya tano kuondokana na mikataba ya kifisadi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom