Tanesco yaja na teknolojia mpya ya LUKU

Tanesco yaja na teknolojia mpya ya LUKU

KIROJO

Senior Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
169
Reaction score
21
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), linatarajia kuanza kutumia teknolojia mpya na ya kisasa zaidi ya ukusanyaji ankara kwa watumiaji wa kati.

Meneja Uhusiano wa shirika hilo Badra Masoud, alisema jana katika taarifa yake kuwa lengo la kutumia teknolojia hiyo, ni kukabiliana na upotevu wa mapato.

“Shirika limefanikisha kupata teknolojia ya kisasa zaidi ya Automatic Meter Reader (AMR) ambayo itaanza kutumika mwaka huu,” alisema Masoud katika taarifa hiyo na kuongeza:

“Mita hizi mpya zitaunganisha teknolojia ya AMR na ile ya LUKU ambapo mteja atalipia umeme kabla ya kutumia na shirika litaweza kupata taarifa ya matumizi ya mteja pamoja na mwenendo wa mita kwa wakati. Hii itasaidia kuongeza mapato ya shirika na kudhibiti upotevu wa umeme.”

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa, teknolojia hiyo ni ya kisasa na itasaidia kupunguza makosa ya kibinadamu, yaliyokuwa yakitokea wakati wa uandaaji wa ankara na usomaji wa mita.

Ilisema kuwa, teknolojia ya AMR inawezesha kusoma na kurekodi matumizi ya umeme kila saa kwa usahihi mkubwa.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, mita za AMR hupeleka taarifa za usomaji wa mita kwenye kompyuta za shirika zilizopo makao makuu kila baada ya saa.

“Mfumo wa kompyuta za AMR hupokea na kuratibu taarifa za matumizi ya umeme kutoka kwenye mita ya mteja na kuandaa taarifa mbalimbali,” ilieleza taarifa hiyo:

“Mteja anayetumia mita za AMR anaweza kupata taarifa ya matumizi yake ya umeme wakati wowote anapohitaji taarifa hizo kwa kutumia tovuti ya Tanesco
swali kwa tanseco ,mlisema hamna hela za uendeshaji sasa hii mladi ni wanini maana mlikuwa mnataka kupandisha bei ya umeme,sasa mimi sipingi technolojia alkini hizo pesa za mradi zitatoka wapi,hii ndo mzingo munayojitwika bila sababu,wewe mapato mmeshandwa wapi kukusanya wakti watu LUKU ndo solution ya hayo.
swali ala pili huu mradi wa AMR hauna ubaya wake vipi
Loss of privacy yaani haina usiri mtu yoyote anaweza akahang nakufanya chochote juu ya meter hizi,
vipi kuhusu
Meter readers losing their jobs-wale wanosoma meter kazi zao vipi mmewahakikishia kazi zote maana hapata kuwa tena na watu special wa kusoma meter ,kitengo kinakufa au?
vipi kuhusu
Increased security risks from network or remote access[SUP]https://www.jamiiforums.com/#cite_note-ieee-6[/SUP]-ulinzi kwenye vituo vya kupokea taarifa upo kama tu transformer kwenye wizi wa mafuta mlishindwa vipi meter amabazo ndo zitakuwa nyingi kuliko transformer?
Naona niishie hapo maana kunavitu hii nchi inawakubalia watu kuingiza taasisi za serikali mambo magumu mwishoe mladi unakufa ,
kuna mambo ya uandilifu na umakini,yaani realibilty na greate potential for monitoring ,hii ni watu wandilifu kitu amabacho hapo tanesco tumeona mawaza uza mengi
Haya nipeni majibu yangu

source Mwananchi la leo.
 
Tayari kuna watu washajihakikishia ten percent hapo!
Kwanza hizi meter walitakiwa wakazifunge kwenye taasisi za serikali ambao ndio wadaiwa sugu wa umeme.
 
Wako makini kuvumbua njia ya kumdhibiti mteja lakini hawataki kuboresha huduma, hopeless..!
 
Mimi kama Mdau wa ICT sioni mantiki ya hiyo system unless wanataka baadhi ya watumiaji wa umeme watabaki kuwa ni wale wa Pay After Use. Kubadilisha mita zote Nchini ni kamradi kazuri, ajabu yake mtasikia watumiaji wanatakiwa kuzilipia tena hizo mita mpya kwa gharama ambazo zitalingizwa moja kwa moja kwenye matumizi yao
 
Automatic Meter Reader in homes could be hacked

Plans to electricity Automatic meters reader in every home by 2020 pose a "national cyber security risk" because the devices could be hacked into, one of the government's own data security consultants has warned.

However, Automatic meter reader can be infected with a 'worm', similar to the viruses that attack personal computers, which can spread from one meter to the whole grid.

Once hacked, the devices could infect Tanzania's entire grid or cause individual customers to be cut off

godwine, which already advises the Ministry of Defence and the Ministry of Justice, hassubmitted its warningto a consultation being carried out by the Department for Energy .
The submission said a automatic reading system in grid would "provide significant benefits to Tanesco [but] may expose the Critical National Infrastructure to a greater degree of risk through cyber-attack. and Automatic metering programmes will disrupted by data protection challenges from customers, civil rights groups and politicians.
It also says consumers are "at risk of unfair, excessive, inequitable and inefficient charging" because Tanesco could use the new data to introduce more complex tariffs to maximise profits at peak times

Tanesco wenyewe Watakuwa wa Kwanza kuchakachua hii teknolojia Yao Mpya.
 
Badala ya kuongeza vyanzo vya umeme, wao wanatafuta namna ya kuwalima watumiaji zaidi na zaidi.
 
this technology is too big to tanesco, sijui walimuhusisha nani kuanalyze hii proposal.. it's stupid idea in 2012 yaani within 5 mins tayari nimeshapata njia 3 za kuihujumu
 
luku zenyewe hazijaeleweka sasa AMR kazi tunayo na hapo watu walishatoa warn kwamba unaweza hack huu mradi usijekuwa topic bungeni...
 
ITs very Sad ,nchi haina umeme ktk kila kaya,halafu tunafikiria kuwa na AMR,marekani watu wengi wamezikataa hizi mita.tatizo no2 watanzania hatupendi kupinga vitu vipya kwa vitendo,huwa tunasema tu ,baada ya wiki mbili tatu,utaona tunakubali kufungiwa hizo mita.
mimi nachofurahia nitaweza kupata umeme wa bure sasa,kwani najua hapo ndo mwazo wa vishoka wa IT,kuvuna.
 
Hazitasaidia sana kupunguza upotevu wa umeme, kwa sababu wanaosababisha upotevu ni miongoni mwao (wizi)
 
Huo ni ulaji mwingine, kwani luku zina matatizo gani?
 
Mimi kitu chochote kinachohusisha mtandao wa komputa kwa tanzania huwa kinanipa mashaka sana hizi bili za kawaida tu huwa tunapanga foleni zaidi ya masaa 6 kwasababu komputa zinasumbua hakuna network sasa mfumo mzima uendeshwe na komputa sijui itakuwaje.
 
Automatic Meter Reader in homes could be hacked

Plans to electricity Automatic meters reader in every home by 2020 pose a "national cyber security risk" because the devices could be hacked into, one of the government's own data security consultants has warned.

However, Automatic meter reader can be infected with a 'worm', similar to the viruses that attack personal computers, which can spread from one meter to the whole grid.

Once hacked, the devices could infect Tanzania's entire grid or cause individual customers to be cut off

godwine, which already advises the Ministry of Defence and the Ministry of Justice, hassubmitted its warningto a consultation being carried out by the Department for Energy .
The submission said a automatic reading system in grid would "provide significant benefits to Tanesco [but] may expose the Critical National Infrastructure to a greater degree of risk through cyber-attack. and Automatic metering programmes will disrupted by data protection challenges from customers, civil rights groups and politicians.
It also says consumers are "at risk of unfair, excessive, inequitable and inefficient charging" because Tanesco could use the new data to introduce more complex tariffs to maximise profits at peak times

nimekukubali kwa tafiti zako , kama Tanesco wakikupuuza muda ukifika watakukumbuka
 
Back
Top Bottom