TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

Safi, hii ni good move.

Je huo umeme utakuwa bei nafuu?, Au ndo yaleyale ya Maharage Chande kutaka umeme uendekee kuwa ghali?
 
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..

My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.

January hapa umepatia!
Ila sasa ifikie hatua sera iruhusu wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa ziada wauze Tanesco kwa makatano kwenye units.
Hii itatengeneza energy mix nzuri badala ya kutegemea juhudi za serikali peke yake!
 
Hizo siasa bwana mdogo umeme wa Maji bado unatumika na ni tegemeo kwa nchi nyingi Duniani .
Umeme wa maji unatumika ndiyo lakini tunakoelekea na haya mabadiliko ya tabianchi tegemea msuguano mkubwa kwenye mahitaji na matumizi ya maji!
Hivi si unakumbuka harakati za kupambana na waliochepusha maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji??
Sasa hizo harakati zitaongezeka as we go!
 
But gharama ya kuzalisha Mwh 1 ni $20-40 hiyo pesa ni kama kubwa kidogo .ukichukulia solar ndio umeme wa bei rahisi duniani .

Umeme wa maji unatumika ndiyo lakini tunakoelekea na haya mabadiliko ya tabianchi tegemea msuguano mkubwa kwenye mahitaji na matumizi ya maji!
Hivi si unakumbuka harakati za kupambana na waliochepusha maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji??
Sasa hizo harakati zitaongezeka as we go!
China wamemaliza kujenga largest hydropower source duniani ,Tanzania uwe umeme wa kizamani kwa sasa ?
 
Baada ya hiyo gharama je kuna malipo ya kila siku wikinau mwezi? Na kwa muda gani ukomo wake? Au unakuwa wa kwetu jumla?

Najaribu kuwaza mitambo tunalipia sisi na huduma tuje lipia sisi tena?

B215 ni nyingi sana

Kwa bilion 20 wangeweza kufanya instalatiin ya kila nyumba hapo umeme wa solar tena ile super kabisa
 
Siyo mbaya...make hapo ni kama panels 125,000 ambayo ni sawa na Bilioni 62. Ukiongeza na storage batteries bank...cabling system pamoja na kujenga msongo wa kuinganisha kwenye line ya kuisafirisha. Naona gharama inakuja hapo.

Shida ni je tumejiandaa kwa ajili ya kuitunza na kubadilisha panels kwa muda muafaka? Make kwa uchafuzi huu wa TANESCO sijui....??
Tunamtengenezea afu anatuzia umeme

Hahahahah noma sana

Kwa hizo gharama ilipaswa mitambo iwe mali yetu chini ya shirika la umeme la nchi
 
bwawa la nyerere halijaisha tumehamia kwenye umeme wa jua.hzo hela si mngepeleka bwawa la nyerere.mbona mnachezea hela.miradi hamumalizi mnarukia mingine
 
Chande akihojiwa na wahariri alisema umeme wa bwawa hautoshi kuleta mapinduzi ya viwanda,akatolea mfano wa Mgodi wa GGM pekee kwamba utatumia megawatt za Mikoa 3 Kwa pamoja Sasa Wakiwa na migodi 10 Kuna umeme?
Pia alisema kusafisha chuma kile Cha Liganga inahitaji megawatt 700 na mbaya zaidi umeme wa Mwalimu Nyerere hauingii kwenye grid Kwa pamoja Bali utaingia Kwa awamu yaani 700*3 .
Atutajie mikoa hiyo mikoa mitatu
 
Bilioni 275 nimpesa kidogo kwa tanesco kwa nini isiwe watafute mkandalasi wa kufunga mitambo ikawa mali yatu badala ya kuuziwa umeme
 
Energy mix, huwezi tegemea Maji tu ikitokea hitilafu nchi itaingia gizani tuanze kulalamika hujuma!!

Ila kuhusu wao kununua ni hoja nzito, ilipaswa huu uwe mradi wao sio Tena wanunue then watuuzie wateja wa mwisho.
Na nani kabisha kuhusu energy mix ? Tanzania tunategemea maji pekee ? Hakuna Solar at household level ? Hakuna Gesi ? tunatumia mpaka mafuta na generator kwa gharama kubwa sana inayopelekea wananchi na nchi kufanya uzalishaji kuwa wa gharama; anyway haya mambo ya energy mix na the only way ya kufanya solar feasible nilishayaongelea hapa....

Chande akihojiwa na wahariri alisema umeme wa bwawa hautoshi kuleta mapinduzi ya viwanda,akatolea mfano wa Mgodi wa GGM pekee kwamba utatumia megawatt za Mikoa 3 Kwa pamoja Sasa Wakiwa na migodi 10 Kuna umeme?
Pia alisema kusafisha chuma kile Cha Liganga inahitaji megawatt 700 na mbaya zaidi umeme wa Mwalimu Nyerere hauingii kwenye grid Kwa pamoja Bali utaingia Kwa awamu yaani 700*3 .
Huku ndio kuhesabu vifaranga wakati hata kuku hauna let alone mayai....; haya mambo ya kutosha tutaendelea kuongezea cha maana ni kumaliza mradi mmoja baada ya mwingine sio kushika shika hapa na pale in the end hakuna kinachofanyika.....; Miradi Lukuki utafikiri kuna mashindano ya kuanzisha miradi badala ya kumaliza tunayoanza hatua kwa hatua
 
Hivi ni Kwa nini nguvu moja isielekezwe sehemu moja ili ikikamilika ianze sehemu nyingine? Hata uangalizi unakuwa makini kwa hao contractors. Bwawa la Nyerere na Umeme wake wa maji na size ya source ya Umeme tuliambiwa shida ya Umeme itakuwa ni history likikamilika percent % sasa hizi source nyingine mpya za nini wakati ili bado? Anyway labda uelewa wangu ni mdogo.
 
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..

My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.

Kwani ule mradi wa upepo umeishia wapi??
 
Ivi huu umeme usiku inakuwaje?
Ndio maana unahitaji storage (battery) kitu ambacho mpaka sasa ndio bottleneck ya solar; tatizo la umeme ni efficient kama unazalisha na kutumia kwa wakati huo huo; generator unaweza kuzima mitambo Hydro unaweza ukapump maji juu kuyarudisha (ikiwa off-peak ili utumie peak time)....; solar you need a good storage au itumike kama mix ya nishati nyingine au uitumie directly unapozalisha
 
bwawa la nyerere halijaisha tumehamia kwenye umeme wa jua.hzo hela si mngepeleka bwawa la nyerere.mbona mnachezea hela.miradi hamumalizi mnarukia mingine
Kwani kabla ya bwawa kulikuwa hakuna miradi mingine ya uzalishaji umeme?
 
Ndio maana unahitaji storage (battery) kitu ambacho mpaka sasa ndio bottleneck ya solar; tatizo la umeme ni efficient kama unazalisha na kutumia kwa wakati huo huo; generator unaweza kuzima mitambo Hydro unaweza ukapump maji juu kuyarudisha (ikiwa off-peak ili utumie peak time)....; solar you need a good storage au itumike kama mix ya nishati nyingine au uitumie directly unapozalisha
Hakuna Cha storage acha kukurupuka,utaingia kwenye matumizi Moja kwa Moja
 
Back
Top Bottom