TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

TANESCO yasaini mkataba wa kuzalisha Umeme Jua MW 150 Kwa Bilioni 275. Waziri Makamba apiga marufuku mauziano ya Umeme kwa Dola

Issue sio kuzalisha hata Jangwani wanaweza kuzalisha kuzalisha ma_gigawatt let alone Megawatt issue ni tunazitunza vipi hizo megawatt ili wakati hakuna jua tuzitumie ? (Storage bado ni bottleneck kwenye solar)

Kwanini wanunue ili wauze ?, Kwanini wazimalize Bwawa la JKN haraka na lianze kazi ili badala ya kununua wao ndio wauze ?
Wenye uelewa mdogo ktk hili watapinga hoja yako.
 
Hizo ni akili za darasa la pili.
Energy mix ni energy security na Tanesco inalenga kuwa na megawatt 5000 by 2025 Sasa bwawa ndio litafikisha 5,000?
Mbona hoja za msingi hujibu

Je tunalipa hiyo gharama ya mutambo pamoja na installation

Swali au hoja kwann visiwe vyetu kwa pesa hiyo?

Au je baada ya b215 kutakuwa na malipo ya uendeshaji au ndo tunamaliza hapo?
 
Tulipe Kwa lipi,sikilizeni video hapo Juu ..

Tanesco ni kutoa guarantee ya kununua Umeme basi
 
Kwani mimi ndo nimeelewa vibaya, mimi nadhani tumempa kandarasi ya supply and installation alafu anatukabidhi then sisi tunaendelea na operation.
Solar system initial installation cost ndiyo kubwa lakinj operation huwa ni kidogo sana.
Hapana kwa maelezo mitambo inakuwa chini yake na ndio maana selikal wanakuwa wateja tena kupitia tanesco
 
Gharama za kuzalisha umeme wa jua ni kubwa ukilinganisha na gharama za kuzalisha umeme wa maji. Huu u.eme wa jua / upepo ni miradi ya kifisadi
 
Serikali Kupitia Tanesco imeandika Historia ya kusaini mkataba wa Kuzalisha Umeme wa Juna na kampuni ya China wenye thamani ya Shilingi Bilioni 275 ambao utazalisha megawatt 150 Kishapu ,Shinyanga na Kwa awamu ya kwanza Wataanza na megawatt 50.

Waziri wa Nishati January Makamba akishuhudia mkataba huo amepiga marufuku Tanesco kununua Umeme kutoka Kwa wazalishaji Kwa malipo ya dola badala yake Shilingi ndio ittumika..

Aidha amewataka Tanesco kuwawezesha wazawa Ili waweze kuzalisha umeme akisema hakuna maajabu Hadi wao washindwe..

My Take
Hongera sana Makamba,majungu achilia failures wewe endelea kuchapa kazi.

=======

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nishati amesema kuwa “kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa, nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu.”

Ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo wa Jua ni jitihada za Serikali za kuhakikisha inatengeneza mchanganyiko wa umeme wenye afya katika gridi ya Taifa ambao utatokana na vyanzo mbalimbali kama vile maji, gesi, upepo na Jua ili hata pale chanzo moja kinapotetereka, vyanzo vingine vitaendelea kuzalisha umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa, ili kuongeza zaidi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati jadidifu, Serikali inakuja na Sera mpya ya Nishati Jadidifu (iko kwenye maandalizi) ambayo itasaidia nchi kuongeza uwekezaji kwenye eneo hilo kwani fedha nyingi duniani, masoko ya mitaji na teknolojia mpya zinajielekeza kwenye nishati jadidifu.

Ameongeza kuwa, kwa sasa kazi inayofanyika pia ni kuainisha maeneo yaliyo na rasilimali ya nishati jadidifu na kipaumbele kitakuwa kwa wazawa kuwekeza kwenye miradi kama ya Upepo na Jua na Serikali itawaunga mkono na kwamba Serikali itakuja na muongozo wa utekelezaji wa suala hilo.

Ameongeza kuwa, kwa maeneo yaliyo nje ya gridi kama vile visiwa, bado Serikali itaendelea kuwezesha jitihada za kupelewa umeme kwa kutumia miradi ya nishati jadidifu kama vile Jua na Upepo.

sawa vip kule bwawa la mwalimu linaendeleaje ujazo wa maji hauruhusu umeme kuwashwa
 
Wewe kiazi kweli, garama ya vitu, unaangalia vitu vingi... Kwanza angalia water fall yake ipoje, angalia kina cha maji, na wingi wa maji
Ndio maana nakwambia wewe ni mpumbavu,unapolazimisha kwamba bil.275 zinaweza uzalishaji umeme megawatt 150 una akili timamu?
 
Ndio maana nakwambia wewe ni mpumbavu,unapolazimisha kwamba bil.275 zinaweza uzalishaji umeme megawatt 150 una akili timamu?
Nina akili timamu kwa maana nafanya kazi kwenye power plant... So naelewa kila kitu..
 
Nina akili timamu kwa maana nafanya kazi kwenye power plant... So naelewa kila kitu..
Unaweza kuwa fundi tuu ,Kwa hiyo unaelewa kwamba Bil.275 zinaweza uzalishaji megawatt 150 za umeme wa Maji? 😁😁

Kama unaelewa Kwa nini hukushauri huko unakofanya kazi mfanya vinginevyo?
 
Issue sio kuzalisha hata Jangwani wanaweza kuzalisha kuzalisha ma_gigawatt let alone Megawatt issue ni tunazitunza vipi hizo megawatt ili wakati hakuna jua tuzitumie ? (Storage bado ni bottleneck kwenye solar)

Kwanini wanunue ili wauze ?, Kwanini wazimalize Bwawa la JKN haraka na lianze kazi ili badala ya kununua wao ndio wauze ?
Unadhani mgt 2100 ni nyingi Kwa viwanda vikubwa? Kuna viwanda vya kuzalisha vyuma vinahitaji mgt 3500 kwa nchi kama ya kwetu ili tuwe na viwanda vikubwa tuwe na mgt 10000 mpaka 35000 ndiyo tutaweza hata kuuza umeme mkubwa
 
Walijinasibu Nyerere dam soon litakuwa tayari na litatatua na kumaliza kabisa shida ya umeme.
Sasa why urukie huko kwenye solar au kuna 10% yako huko na hisa kiasi kadhaa..?
Halafu umeme wa solar gharama yake ipo kwenye maintenance yaani kubadili panels, wiring, batteries.
 
Unaweza kuwa fundi tuu ,Kwa hiyo unaelewa kwamba Bil.275 zinaweza uzalishaji megawatt 150 za umeme wa Maji? [emoji16][emoji16]

Kama unaelewa Kwa nini hukushauri huko unakofanya kazi mfanya vinginevyo?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]... Ila huku hamna wapigaji...
 
Unaweza kuwa fundi tuu ,Kwa hiyo unaelewa kwamba Bil.275 zinaweza uzalishaji megawatt 150 za umeme wa Maji? [emoji16][emoji16]

Kama unaelewa Kwa nini hukushauri huko unakofanya kazi mfanya vinginevyo?
Inaweza mbona, kamamna water fall yenye uwezo wa kuzungusha turbine yenye kufua kiwango hko cha umeme
 
Back
Top Bottom