Hivi mnauelewa utaratibu wa manunuzi ya umma? Ni wapi katika kanuni hizo zinasema wanafunzi au wakazi wa kiTanzania walioko nje wanaweza kutumiwa kunua vifaa vya Serikali/Shirika kinyume na taratibu hizo?
Kama kweli mnuwezo huo leteni tenda!!
Tk,
Nadhani wewe ni mmoja wa watu waloshindwa jua maana. na hunipa shida sana kujieleza zaidi kwa sababu ni wewe unatakiwa kusoma na kuchambua yaliyomo baina ya kila mstari.
Uwezo wa kujua wapi mali inapatikana ndio tunasema sisi tunao, na sii uwezo wa kushiriki ktk tender za serikali ambazo zinahitaji mabillioni ya fedha. Kisha in reality najua siwezi kupata kutokana na ukiritimba..kifupi haiwezekani..
Hivyo mnapowataka vijana wawe preactive wakati mkijua hatu qualify ktk utaratibu wenu wa manunuzi, kisha mnakuja na kuuliza kwa nini hatushirki mnataka sisi tujibu vipi?..
Hizo taratibu kaziweka nani, sisi au ni serikali ktk kujenga bureaucracy na mwanya wa corruption. Tazama mfano mdogo wa Tazara wao wanaenda moja kwa moja GE wakati Tanesco wanapitia wizarani..now who finance Tazara kama sio serikali za nchi mbili iweje kule iwe rahisi lakini tunashindwa Tanesco na hata TRC..
Mkuu nitakwambia kitu kimoja huyo msomi mliye msomesha hadi chuo kikuu ni mtaji mkubwa ktk maendeleo ya Tanzania kuliko mwekezaji wa billioni moja..mkishindwa kuwatumia makosa sii yangu mimi ila yenu kwa tamaa ya fedha na ulimbukeni ndio maana mnaweza sheria na taratibu sizizokuwa na kichwa kabisa..We can help, lakini taratibu za serikali zinataka ati Mtanzania aje na dollar laki moja kuwekeza nchini ndio apewe kibali cha excemption lakini akija na degree yake hana thamani, yet rais huyo huyo anawataka Watanzania warudi nyumbani kuwekeza, kuwekeza katika kitu gani?.....Unafikiri huyu rais anafikiria kitu gani zaidi ya kuwekeza ni miradi ya fedha tu.. Wasomi vijana wake waliofuta madarsa wakahifadhi misahafu ya elimu dunia hawa qualify!..why?...hivi elimu za hawa vijana mnaona hazina impact kabisa ktk utaratibu wa maendeleo yenu...mnaichukulia elimu kama sii investment wala haipo ktk Rights za wananchi isipokuwa ni privilege fulani hivi...
Nitakupa mfano mwingine nimeona TRC wameweka tender ya kuwa supplied vyuma vya reli...Mimi najua wapi wanaweza kuvipata na hata shirika gani lionaweza kutandika reli na ukarabati wake kwani ndio kazi yao kubwa hata huku Nje.Wanaaminika na wanafanya kazi ya Uhakika.Lakini nitaweza vipi kuishauri serikali ambayo haina hata idea ya mashirika yanayotengeneza au ku supply vyuma hivyo acha mbali utendaji kazi wake... nitaanzia wapi?
Leo wanatoa tender ati washiriki wanashindana kuandika Bidding Documents kwa kiingereza wakati najua fika huyo Waziri na wakurugenzi wake watatoka watupu kama sii kuwategemea wataalam wa TRC.. Then kwa nini TRC wenyewe wasitafute mali hiyo na kuwakilisha mapendekezo yao wizarani.
Mkuu wangu tender inapendeza tu ikiwa unatafuta ku contract kazi nzima kwa shirika mwekezaji na sii kwa mali uhayotaka kununua kwa mahitaji yako..besides hata siku moja serikali zetu haijawahi kununua wala kufuata tender hahisi na Imara isipokuwa ghali na yenye ulaji iwe magari, rada, ndege U name it kila siku tunanunua vitu ghali kuliko thamani halisi ya vitu hivyo... Yoote ni NJAA tu mkuu wangu hatuna sababu, hizi siasa nyingi za utaratibu na kadhalika ni kujipa moyo wa U saint!