Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Zitto,
Ur not serious!.. are You?
Mkuu tulikwambia toka siku zile kwamba mitambo ipo na sii GE peke yake mipya na kukukuu maadam wapeni kazi vijana wataifanya..Mimi binafsi nilikwambia pia kabla na baada ya mgogoro wa Dowans...nimeandika humu humu JF iweje leo somo tunarudia kule tulikotoka?..
Acha mbali kwamba Lowassa alipotembelea hapa (hatukuonana naye alikwenda Mexico badala ya kukutana na Watanzania)niliwajulisha baadhi ya viongozi walioandamana na msafara wake, lakini Richmond ilikuwa ndio somo na hakuna upinzani.
Sasa nenda kawaone hao Tanesco wambie vijana wapo tayari kisha rudisha kazi hiyo hapa JF utaona uwezo wa vijana mnapowapa kazi ya taifa...
Binafsi siwezi kwenda ovyo kutafuta mitambo kisha majibu yenu yawe yale yale tunaonekana wajinga na matapeli.. ongea na Tanesco watupe go ahead, contact zao hata iwe kupitia kwako tutaifanya kazi tena haraka kuliko mtakavyo fikiria.
Kisha gharama ya ujenzi haiwezi kuwa kubwa kwa sababu ile mitambo ya Richmond/Dowans tayari ilikwisha jengewa na kufanya kazi hivyo chochote mtakachonunua kitawekwa pale ilipokuwa mitambo ya Dowans au sio!.
kuharibika kwa mtambo wa Songas UGT1 (20 MW), kuharibika kwa mtambo wa Kihansi (60 MW) na kuharibika kwa mtambo wa Hale (8 MW).
Tk,Hivi mnauelewa utaratibu wa manunuzi ya umma? Ni wapi katika kanuni hizo zinasema wanafunzi au wakazi wa kiTanzania walioko nje wanaweza kutumiwa kunua vifaa vya Serikali/Shirika kinyume na taratibu hizo?
Kama kweli mnuwezo huo leteni tenda!!
Hivi kweli utaratibu wa manunuzi ya umma mnauelewa? Ni wapi katika taratibu hizo unawaruhusu Serikali/Tanesco kuwatumia wanafunzi au waTanzania waliopo nje kufanya manunuzi kinyume na taratibu? Utaratibu huo ulioelezwa hapo juu si tu utazua soo jingine?
Kama kweli mnauwezo huo kwanini hamleti tenda?
...halafu ndio mnajiita watetezi wa maslahi ya umma..........!
ulikuwa wapi wakati wa Zabuni ya Richmond......ndugu yangu........
Una maana na wewe unataka kuanzisha Richmond yako au??
Nchi hii kila mmoja anataka kila akisemacho kifanyiwe kazi isipofanyiwa kazi basi adhabu inatupwa kwa wananchi walipa kodi! Kwanini Tanesco wameshindwa kujiwekea mikakati ya kuhakikisha kwamba umeme unapatikana bila tatizo? Umeme wenyewe unawafikia watu sio zaidi ya milioni 10 tu alafu wanashindwa sasa nchi mzima itapata umeme mwaka gani! Huu ni uzembe wa hali ya juu na hatuwezi kukubali! tanesco wafanye kazi sio siasa!
Zitto,
Umejiingiza sana kwenye masuala ya TANESCO kuliko shirika jingine lolote la UMMA. Hii ni hatari kwako kwani wewe unaongea na MENEJIMENTI tu, undani hasa wa shirika lile hauujui. Iachie Bodi ya TANESCO ifanye kazi yake. Ufisadi uliomo ndani ya TANESCO hakuna siku litakaa litengeneze faida!