TANESCO yatangaza upungufu wa Umeme kwenye Gridi ya Taifa kutokana na Ukame

TANESCO yatangaza upungufu wa Umeme kwenye Gridi ya Taifa kutokana na Ukame

Mi hata siwazi acha mkatiwe hadi mkome.hapa kuna jenereta iko standby ndio raha ya kuishi ushuani!!na bado hii ccm wataanza kuwakamata mmojammoja wawasire na picha ya kikwete iko ukutani..
 
Kwani suala la ukame linadhibitiwa na ilani ya CCM..??
Ndezi Kama nyinyi ndio mtaji wa ccm, kwa hiyo vyanzo vya umeme ni maji tu? Ile gas ya Mtwara unajua ccm wamempa nani? Kuna umeme wa Solar, umeme wa upepo, umeme wa joto ardhi(Geothermal) nk. Ila kwa kuwa ccm na majinga Kama nyinyi uwezo wenu ni mdogo basi subirini tu
 
Mtambo una hililafu, miwili inafanyiwa matengenezo ya kinga.... kwa nini hayo matengenezo kinga yasifanywe kwa mmoja mmoja?
 
Swali : hivi JPM angekuwepo angevumilia haya? Ili uwe kiongozi mwenye impact lazima uwe umejiscrifice maisha bila hivyo wasaidizi wako watakuchezea sharubu .JPM alikuwa sura ya mbuzi ukizingua ana kuzingua kweli kweli mchuna kweupe bila hata chembe ya aibu ndio maana nchi ili nyooka
 
Leo tarehe 22/11/2022 TANESCO wametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuelezea sababu za mgao unaoendelea nchini.
Kwa habari zaidi soma Press release Hapa chini

====

Shirika la Umeme Tanzania limetangaza upungufu wa Megawati 155 za Umeme wa Maji uliosababishwa na Ukame kwenye Mabwawa ya Kihansi, Mtera, Nyumba ya Mungu, Hale na Pangani.

Pia, Mtambo mmoja wa Kidatu unaozalisha Megawati 50 umepata hitilafu na Mitambo miwili ya Ubungo III inayozalisha Megawati 40 ipo kwenye matengenezo kinga, hivyo kupunguza Takriban Megawati 300 za Umeme wa Maji na Gesi.

Hali hiyo itadumu hadi mwanzoni mwa mwezi Desemba 2022 baada ya kumalizika matengenezo na kuongezeka maji kwenye mabwawa pamoja kuingizwa Megawati 225 kwenye Gridi ya Taifa.

View attachment 2424362
Hao Tanesco mim wameshanichosha yani kwanza maelezo yao yamekaa kitapeli tapeli tu
 
Kazi kweli kweli..

Hivi wakati viongozi wengine duniani wanapowaza na kuyapatia ufumbuzi matatizo ya watu wao hawa wetu wanakuwa wanawaza nini?
Kwanza wanawaza masilahi yao binafsi maana Tanzania uongozi ni fursa tu kama fursa zengine, kisha wanawaza masilahi ya chama maana ndio huwafanya waweze kuendelea kutawala na kupata hizo fursa za uongozi , na mwishoni ndio wanakuja kuwaza matatizo ya wananchi wao katika style ya kama kutoa msaada tu na ndio maana utaona wananchi hutoa sana shukurani pale serikali inapotekeleza majukumu yake.
 
Back
Top Bottom