Tanga: Auawa kwa kuchomwa kisu, inadaiwa chanzo kumuomba maji ya kunywa aliyefunga

Tanga: Auawa kwa kuchomwa kisu, inadaiwa chanzo kumuomba maji ya kunywa aliyefunga

Ngasere45

Senior Member
Joined
Dec 31, 2022
Posts
148
Reaction score
566
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia Hassan Nyundo (25) Mkazi wa Kijiji cha Vue kata ya Mowa Wilayani Mkinga kwa tuhuma za kumchoma kisu Amiri Mohamed (30) huku ikidaiwa kwamba sababu mojawapo ya ugomvi ni kitendo cha Amiri kumuomba maji ya kunywa wakati akifahamu kuwa Hassan amefunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

RPC wa Tanga Henry Mwaibambe amesema kuwa 05/04/2023 majira ya saa sita mchana Amiri na Mtuhumiwa walikuwa wakiishi nyumba moja hivyo hadi mauti yanamkuta Amiri alimshinikiza Mtuhumiwa kumpatia maji ya kunywa kitendo kilichomchukiza Hassan (Mtuhumiwa) na kusababisha ugomvi uliopolekea kumchoma kisu kulichosababisha kufia njiani wakati akiwahishwa Hospitali.

Kamanda Mwaibambe amesema hadi sasa kuna taarifa mbili juu ya tukio hilo ambapo wengine wanasema Mtuhumiwa alichukizwa na kitendo cha Amiri kumuomba maji pamoja na kunywa maji wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani lakini wengine wanasema ni ugomvi wa kawaida.

“Kwakweli hadi sasa chanzo kamili cha tukio hilo bado hakijajulikana kwani hawa wawili ni ndugu waliokuwa wakiishi nyumba moja, ni mauaji ya kusikitisha sana haiwezekani ugomvi wa maji tu unachomoa kisu una mchoma mwenzako, kwakweli huu ni mmomonyoko mkubwa wa maadili”

Millard Ayo
 
Mwili usiojishughulisha ni hekalu la shetani, wangekuwa kwenye vibarua au shambani wanapalilia wangepata wapi muda wa kuchomana visu?
Wanakula wanashiba, energy haina matumizi matokeo yake wapata nguvu za kupigana.
 
Kuomba maji tu kusababishe kumchoma kisu!! Rest in peace Amiri
 
Huyo ni mpumbavu sana ndio wale hawajawahi fika hata madina huko kutalii.

Kuna wajinga wengine nimepishana nao wameziba njia/barabara wamebebelea sijui nini huko wanaita njia ya msalaba

Ujinga ujinga ujinga
 
kama ni kweli amemchoma kisu kisa kuombwa maji,
Basi hawa ndugu zetu huwa wanatumia nguvu kubwa kutetea hiyo dini yao

dini iliyo safi inawahimiza watu kupendana
pasipo upendo hakuna dini ya kweli

RIP Amiri
 
Back
Top Bottom