Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara ya madanguro maarufu kama madada poa inakoma mara moja Jijini humo.
DC Mganndilwa alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha cha baraza la madiwani wa halamashauri ya jiji la Tanga ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni Sabasaba na barabara ya Uhuru na kusema kuwa wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine.
"Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna, madanguro ambayo dada zetu wanajiuza naomba nitumie hadhara hii kwakuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati nikifanya opereshen zenu basi mshughulike na watu hawa, "alisistiza DC Mgandilwa.
Katika hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na migogoro isiyokuwa na lazima.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amewataka wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo.
"Nitoe angalizo kwa wakuu wetu wa idara na watumishi wote wa halmashauri wapatao 3000 waelewe kwamba kikao cha mwisho chenye maamuzi katika jiji hili ni baraza la madiwani hivyo wasijaribu wala wasiwaze kujikweza kimadaraka hakikisheni sheria kanuni taratibu na miongozo zinafuatwa ili tusifikie kwenye migongano, "alisistiza Meya Shiloo.
Mkurugenzi wa jiji la Tanga Spora Liana amesema Halmashauri hiyo itatoa taarifa ya kila matumizi ya fedha yanayofanywa kwa wananchi lengo ni kuweka wazi kwa kila mwananchi kufahamu fedha za maendeleo zinazotolewa kwenye maeneo yao.
anataka ukahaba ukimeshwe? sishabikii ukahaba na siungi mkono ukahaba lakini amesahau kuwa hao anaowaona mitaani ni mahakaba masikini na madhara yao ni madogo. kuna makahaba huku maofisini, hao wanawake wanaojifanya wasafi na wasomi, wanauza miili yao kuliko hata hao. ukiona mtu anajitembeza barabarani ni kahaba masikini hana namna.
hao hao wanawake wanaojifanya wazuri wa mjini na wasomi, ukishika namba yake amesevu majina rundi ya wanaume wa kuwapanga. A1, A2, A3............, B7..........Z....., mara fundi nguo, fundi bomba, fundi gereji, fundi ujenzi, bajaj, boda, taxi kariakoo, taxi sinza, taxi ubungo......, fundi computer, fundi simu....etc. hao mafundi wote wana professions zao hata sio mafundi wala nini. zamani zangu za ujinga, niliwahi fumania simu ya kibenten mmoja, hadi stim ziliisha. ni hatari. wanaume tunapanga, ukiona hasa weekend anakwambia atafua nguo hadi saa kumi na mbili, jua mwingine amemwambia atafua hadi saa kumi, mwingine hadi saa tisa, mwingine hadi saa saba, mwingine hadi saanne, na wanajua kuchunga mda hao, muda ukifika anakwambia anawahi nyumbani mamake anamuhitaji kumbe anawahi foleni.