Tanga: Kiwanda bubu cha silaha chabainishwa

Tanga: Kiwanda bubu cha silaha chabainishwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Msako wa polisi wanasa kiwanda bubu cha silaha

KIWANDA cha kutengenezea bunduki za kienyeji aina ya gobore kimegundulika baada ya msako mkali kuendeshwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja anayehusika na kutengeneza vifaa hivyo pamoja na bastola aina ya Trurus ambayo imetengenezwa nchini Marekani iliyokuwa inamilikiwa bila kibali halali ikiwa na risasi tano pamoja na magazine yake.

BUJNDUKI.jpg

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP, Safia Jongo, wakati akitoa taarifa ya mwezi Oktoba, mwaka huu.

"Operesheni ilipangwa kimkakati tumekuwa na matumizi mabaya ya silaha hizo aina ya gobore katika misitu yetu, ilitulazimu kupanga mikakati kujua ni wapi yanapotoka," alisema ACP Jongo.

"Tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja mwanamume ambaye alikuwa na mtambo wa kutengeneza hayo magobore, lakini akiwa na magobore 11, mbali na magobore hayo pia alikuwa na vifaa vya kutengeneza silaha, kama trigger, cocking handle ambayo inatumika katika silaha hizo," alisema Jongo.

Pia katika msako huo walikamata bastola aina ya Trurus ambayo imetengenezwa nchini Marekani ambayo ilikuwa inamilikiwa isivyohalali na ilikuwa na risasi tano na magazine yake.

Kadhalika, kwenye operesheni hiyo wamekamata kilo 372 za mirungi pamoja na pikipiki 12 ambazo zilikuwa zikisafirisha mirungi na wahamiaji haramu," alisema Jongo.

NIPASHE
 
Kijijini ukiwa na gobore unaheshimika sana. Ulinzi na kuwindia
 
Mbona ni kitu Cha kawaidi,huyo ni fundi mchundo anatengeneza shoka tezo ,mapanga nk
 
Hawa watu walipaswa wakusanywe sehemu moja wafunguliwe kiwanda tupate silaha zetu, lakini tunavyojua kuzikatikia bilateral agreements za mabeberu ili watupe mikopo tukanunue silaha kwao lazima hawa ma expert tuwaite magaidi na wakosaji.
 
Back
Top Bottom