PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Wanakijiji 10 wa kijiji cha Chang’ombe kilichopo kwenye kata ya Segera wilayani Handeni wamefariki dunia kwa kugongwa na lori lililopoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari ndogo aina ya Tata.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian lori hilo liliwagonga watu hao usiku wa kuamkia leo Januari 14, 2025 na kusababisha vifo hivyo sambamba na maheruhi.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo hiyo.