Tanga: Lorry laua watu 10 waliokwenda kushuhudia ajali Segera

Tanga: Lorry laua watu 10 waliokwenda kushuhudia ajali Segera

Watu wameshabeba chao,kaangusha kadogo akajua mtajileta tu barabarani awafyeke vzur

Magar makubwa yenye watu wengi yamemshinda
 
Dah,wamekufa kifo cha maumivu makali sana, naogopa sana kifo cha ajali Mungu atuepushie kwakweli,roho inatoka kwa maumivu makali, wema wao wakutaka kutoa msaada umewaghalimu uhai. Walale pahala pema insh.
Wengine hawana wema wanafika wanawavua hadi saa na mikanda waliyovaa majeruhi yaan watu wengine ni makatili zinapotokea ajali ni basi tu
 
Wanakijiji 10 wa kijiji cha Chang’ombe kilichopo kwenye kata ya Segera wilayani Handeni wamefariki dunia kwa kugongwa na lori lililopoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari ndogo aina ya Tata.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian lori hilo liliwagonga watu hao usiku wa kuamkia leo Januari 14, 2025 na kusababisha vifo hivyo sambamba na maheruhi.

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo hiyo.

View attachment 3201486
Ajali zina hulka ya kualikana
 
Back
Top Bottom