beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga imewaachia huru wakurugenzi sita wa bodi ya kiwanda cha chai cha Mponde Tea Estate akiwamo mbunge wa zamani wa Bumbuli, William Shelukindo.
Wameachiwa baada ya ofisi ya Taifa ya mashtaka kufuta mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakiwakabili ikieleza kuwa haina nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.
Mbali na Shelukindo aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, wengine ni mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Mbeya, Nawab Mulla ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa Mbarali; mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya ya Lushoto ambaye kwa sasa ni diwani wa Mponde, Richard Mbughuni, Shahdad Mulla, Richard Semroki (marehemu) na Rajab Msagati.
Kwa mujibu wa mwandamizi wa ofisi ya Taifa ya mashtaka Mkoa wa Tanga, Regina Kayuni ameeleza kuwa washtakiwa hao wamefutiwa mashtaka chini ya kifungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Septemba 27, 2018 walisomewa mashtaka yao ikidaiwa kuwa kati ya mwaka 2000 na 2013 walihusika na mashtaka hayo.
Katika shtaka la kwanza linalowahusu Shelukindo, Mulla, Shahdad na Mbughuni wanadaiwa kula njama kwa kuagiza nje ya nchi malighafi ya Sh135 bilioni kwa ajili ya kiwanda cha Mponde pamoja na wakulima wa chai na kisha kudai msamaha wa kodi hivyo kuisababishia Serikali hasara ya Sh30 bilioni.
Shtaka la pili, ambalo liliwahusu washtakiwa wote sita ni kuisababishia Serikali hasara ya Sh30 bilioni kinyume na aya ya 10 ya jedwali la kwanza la kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60 (2) cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 pitio la mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria namba 3 ya mwaka 2016.
Shauri hilo limefutwa leo mahakamani hapo baada ya kufikishwa kwa ajili ya kutajwa tena.
Chanzo: Mwananchi