Pre GE2025 Tanga: Mjumbe wa kamati kuu UWT-Taifa achangia bati 40 kwa familia ya watoto yatima

Pre GE2025 Tanga: Mjumbe wa kamati kuu UWT-Taifa achangia bati 40 kwa familia ya watoto yatima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wakuu naona huu ndiyo ule mwaka wa kupokea, kila mtu anajitia kuchangia hiki mara kile ilmradi tu aonekane atajwe tajwe ili kujiwekea mazingira mazuri.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu UWT Taifa Wilaya ya Handeni Bi Mariam Mwanilwa amechangia Bati 40 kwa familia ya watoto Yatima 6 iliyopo Mtaa wa Zizini Kata ya Chanika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Mabati Hayo, Bi Mariam Mwanilwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Marafiki wapenda Maendeleo Wilaya ya Handeni MMAHA, amesema kuwa baada ya Balozi wa Maji Mkoa wa Tanga Habib Mbota maarufu Moja kwa Moja kumshirikisha kuhusu Nyumba ya watoto hao kuezuliwa na upepo mkali baada ya kubwa kubwa kunyesha aliamua kuunga Mkoani juhudi ambazo alizianzisha za kuwapatia makazi mapya.

" Mimi nilipigiwa simu na Moja kwa Moja kuhusu kuwapatia makazi watoto hawa sita Yatima na kweli nikaona nije hapa na wanawake wenzangu wa UWT kupaona na kukabidhi Mabati haya Ili nyumba iezekwe na watoto wahamie" Alisema Mwanilwa

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom