Tanga: Mkuu wa wilaya Kilindi, Hashim Mgandilwa uwezo wake wa kuongoza unatia shaka

Tanga: Mkuu wa wilaya Kilindi, Hashim Mgandilwa uwezo wake wa kuongoza unatia shaka

Kama una ushahidi na hayo nakushauri uende nao kwenye ofisi iliyo juu yake yaani mkoani...bila kuacha kumpa taarifa OCD wa wilaya ya Kilindi.....ikishindikana huko ndio uje huku
Aje huko wapi!?
 
Kilacmtu akipata upenyo ni kutandika tu

Ova
Ni nafuu angekuwa tu mpigaji lakini amevuka mipaka kwa kulewa madaraka amekuwa mnyanyasaji sana , vitendo anavyofanya kwa wakulima wa huku ni vya kiuonevu , huyu bwana tunajipanga kufanya maandamano kwenda ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na mabango
 
Hii nchi laana tuliyopewa ni hio ya kuteua wakuu wa mikoa na wilaya wakati ilitakiwa waombe kazi kama taaluma nyengine wanavofanya/ wapigiwe kura,
Usingesikia huo upuuzi. Wanavimba.

Katiba mpya muhimu.
 
Hii nchi laana tuliyopewa ni hio ya kuteua wakuu wa mikoa na wilaya wakati ilitakiwa waombe kazi kama taaluma nyengine wanavofanya/ wapigiwe kura,
Usingesikia huo upuuzi. Wanavimba.

Katiba mpya muhimu.
Ni sahihi kabisa nakubaliana na unalolisema Sisi huku kilindi tunateseka Sana na huyu bwana ambaye kwa sifa zake hata ujumbe WA nyumba kumi hawezi kuongoza
 
WaTanganyika hakuna wanachopata ndani ya huu muungano.....na bahati mbaya.....(ngoja niweke akiba)
 
Rais wangu nakusalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mimi raia wako Rashidi Jumaa kutokea Tanga wilaya ya Kilindi ni mzawa wa huku

Sauti ya mnyonge huwa haisikiki kwa urahisi, nimeona nilitoe dukuduku langu humu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kero tuliyokuwa nayo na huyu mkuu wetu wa wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga, Hashim Mgandilwa Nina imani kubwa serikali yako ni sikivu itanipa sikio la kunisikiliza.


Mkuu wa wilaya ya Kilindi ni kichefuchefu

Amekuwa akiwakandamiza sana wakulima na kuonesha upendeleo wa wazi kwa wafugaji bila kusikiliza pande zote

Mfano katika kata ya Mafisa kuna kesi ya mkulima kupigwa risasi na mfugaji na kesi ilifika mezani kwake lakini hakuna maamuzi yeyote aliyoyatoa na kwa taarifa nilizokuwa nazo ana uswahiba na yule aliyefanya tukio hilo la kinyama wana mradi wao wa ufuagaji

Mashamba ya wakulima yanaharibiwa na wakulima wanatengenezewa makosa ya uongo wanawekwa ndani

Sio msikivu kabisa kwa raia wake ametawaliwa na ujeuri / kiburi cha madaraka anafanya ofisi kama ni mali yake hafwatishi kanuni na muongozo wa kazi ,

Ukimfuata ofisini huwa ana majibu ya ovyo sana ya kuonesha dharau kwa sisi wananchi wa hali ya chini

Huyu mkuu wa wilaya naona bado ni mwanafunzi hana uwezo wa kuongoza, hatufai wilaya ya Kilindi Tanga na wala hafai popote pale, maana hata akiamishwa ni sawa na kupeleka matatizo sehemu nyengine.

Ninayozungumza sio majungu ni hali halisi tunayokutana nayo huku. Nakuomba Rais tuma wapelelezi wako wafuatilie utendaji wake watayasikia mambo mengi sana juu yake.
Mkuu niko nje ya mada kidogo naomba nisaidie maelekezo kuhusu io wilaya hivi maisha ya huko yakoje hasa hasa kwenye suala la upatikanaji wa maji majumbani pamoja na umeme na uwepo wa Hospitali karibu je.? ivyo ni vitu vya uhakika au ni changamoto
 
Back
Top Bottom