Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Serikali imesema kuwa imebaini nusu ya vituo vya kulelea Watoto Mchana (Day Care Centers), vinaendeshwa kinyemela pasipo taratibu muhimu za kisheria.
Hayo yalibainika mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya Maofisa kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kubaini kuwa kati ya vituo 68 vya malezi ya watoto mchana, vituo 33 pekee ndivyo vyenye usajili wa kutoa huduma hizo kisheria.
Kufuatia hali hiyo, timu ya Ukaguzi ikiongozwa na Mwakilishi wa Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Miriam Luka, ikalazimika kufunga vituo kadhaa vilivyokithiri na kuvitaka kufuata Sheria na Kanuni za uanzishwaji wa Vituo vya Malezi kwa watoto wadogo mchana.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Ofisa Ustawi wa Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo, Luka alisema vituo vya malezi kwa watoto mchana vinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo chini ya Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inayoelekeza namna ya endeshaji wa vituo hivyo.
"Mimi nazungumza kwa niaba ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii hivi vituo havifai kwa kutoa huduma kwa watoto wetu, mazingira hayafai kabisa tafuteni sehemu sahihi ndiyo muanzishe hivi vituo,"alisema.
Awali, Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo, Dk. John Jingu, akiwa katika kikao kazi na Maofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tanga, aliwaagiza Maofisa hao nchini kukagua na kufuatilia uendeshaji wa vituo hivyo na kuona jinsi wanavyotoa huduma za malezi kwa watoto.
Aidha, aliwataka Maofisa Ustawi wa Jamii nchini kuhakikisha wanasimamia uendeshwaji wa Vituo vya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto mchana (Day Care Centers), ikiwamo kukagua maeneo na huduma zinazotolewa na vituo hivyo ili vitoe huduma stahiki kwa watoto nchini.
"Tusimamie hivi vituo kwa ukaribu watoto wetu wanaenda huko tuangalie mazingira yake yakidhi vigezo vilivyowekwa ili tuweze kumpatia mtoto malezi yanayostahili," alisisitiza.
Kwa mujibu wa Dk. Jingu, Kada ya Ustawi wa Jamii ni muhimu katika kuhakikisha Jamii inajengeka vizuri na kutatua changamoto za jamii husika hasa katika masuala ya saikolojia.
Aidha, alikemea uanzishwaji holela wa vituo vya malezi kwa watoto wadogo bila kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo na kuwataka wamiliki wa vituo hivyo kuzingatia sheria, ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa Vituo hivyo.
Awali, Katibu Mkuu huyo katika kikao kazi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Jonathan Budenu, aliiomba Wizara kuratibu ukaguzi wa vituo hivyo mara kwa mara kwani vituo vingi havina watoa huduma waliokidhi vigezo vya kutoa huduma ya malezi kwa watoto.
Aidha, alimuhakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. Jingu, kusimamia maelekezo yote aliyoyatoa na kuhakikisha yanatekelezwa kwa maslahi mapana ya maendeleo ya mtoto.