Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika na kiukweli Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Anapendwa na watanzania haijapata kutokea,anakubalika na watu sijapata kuona. Watu wanampenda na kumkubali Rais Samia mpaka Wanashindwa kujizuia hisia zao za Upendo kwa Mama.
Mama anapendwa katika hii Nchi kuliko binadamu yeyote yule anayeishi na aliye hai katika ardhi hii ya Tanzania. Haijapata kutokea ,haijapata kuonekana,haijapata kushuhudiwa Rais akipendwa na watu kiasi hiki katika bara hili na pengine Duniani Kwote.
Siyo kwa sababu ni Mama bali ni kwa sababu ni Mama mwenye upendo,huruma, unyenyekevu,ukarimu na moyo wenye kujali na kuguswa na shida za watu. Amegusa maisha ya wengi na ndio maana unaona watu wakiguswa sana na Yeye. maisha yake ni kama yamekuwa faraja ,baraka na Neema kwa watu.
Ndio sababu ya kuona hata katika mikutano yake watu wakimiminika kwa wingi Utafikiri wanavutwa kwa Sumaku na wakati mwingine unaweza kufikiri pengine watu wameisha huko majumbani na wote wapo kumlaki na kumpokea Mama wa Afrika na jasiri muongoza njia.
Mama Samia ni Mpango wa Mungu.siyo mtu wa kawaida huyu Mama. Huu siyo Upendo bali ni mahaba ya watanzania kwa Rais wao.
View attachment 3250294View attachment 3250295View attachment 3250296
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.