Tanga waikatae CCM?

Tanga waikatae CCM?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
CCM ina tabia ya kupeleka miradi mikubwa pale ambako wanakataliwa au Kuna dalili ya kukataliwa. Tanga na wilaya zake ni chimbo la CCM kwa karne na karne, hawana hofu ya kukataliwa hivyo hawapeleki miradi ya maana Tanga.

Tanga hakuna mradi hata mmoja wa umwagiliaji ingawa Kuna wakulima wengi. Tangu hasa kule Handeni ndivyo wilaya ambayo hakuna maji hakuna mito Wala mabwawa lakini CCM haipeleki maji ya mabwawa, bomba Wala kuchimba visima. Kata hazina vituo vya afya kama sera yao inavyosema, kata hazina vituo vya polisi Wala mahakama, hakuna shule za wasichana za bweni kama mikoa na wilaya nyingine; hakuna mradi wa maana Tanga na wilaya zake zote.

Tanga Tanga Tanga kunani? Tanga Wana kasoro gani kwenye kufikiria? au ni kwasababu ya kula sana viporo vya ugali wa mahindi?
 
Mimi ni mkaazi wa Tanga(muhamiaji kutoka Ngorongoro). Kuna siku tulikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji. Mwenyekiti, mtendaji na diwani wakawa wanasema CCM hoyee..! Muda wa maswali ulipofika nikauliza "huu ni mkutano wa hadhara au wa chama?, mbona Kila kiongozi anayesimama anasema CCM hoyee?" Mtendaji akaniambia alikuwa rafiki yangu akaniita akaninong'oneza, "kijana kaa kimya utapotezwa". Nilishtuka sana
 
Screenshot_20250130-072417_Instagram.jpg

Screenshot_20250130-072405_Instagram.jpg

Screenshot_20250130-072355_Instagram.jpg

Screenshot_20250130-072342_Instagram.jpg
 
Handeni Wana English Medium Pre and Primary School
 
Mimi ni mkaazi wa Tanga(muhamiaji kutoka Ngorongoro). Kuna siku tulikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji. Mwenyekiti, mtendaji na diwani wakawa wanasema CCM hoyee..! Muda wa maswali ulipofika nikauliza "huu ni mkutano wa hadhara au wa chama?, mbona Kila kiongozi anayesimama anasema CCM hoyee?" Mtendaji akaniambia alikuwa rafiki yangu akaniita akaninong'oneza, "kijana kaa kimya utapotezwa". Nilishtuka sana
Na wewe ukakubali kukaa kimya. Tanga 100% ni CCM lakini ndiyo 100% maskini.
 
Handeni Wana kabarabara kamoja TU ka lami kamepita pale vuuup hadi korogwe, pale pana kabarabara kamoja TU kamepita pale vuuup kwenda Arusha, pale lushoto Wana kakwao kamepita kutoka pale mambo kakaishia pale Magamba alipojenga mh. Mkapa na Ngwilizi basi kwingine koote ni mashimo na vumbi TU ingawa makabichi yote nchini yanatoka huko. Pale muhema na pangani ndio usiseme kabisa. Ni mandondocha?
Mimi ni mkaazi wa Tanga(muhamiaji kutoka Ngorongoro). Kuna siku tulikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji. Mwenyekiti, mtendaji na diwani wakawa wanasema CCM hoyee..! Muda wa maswali ulipofika nikauliza "huu ni mkutano wa hadhara au wa chama?, mbona Kila kiongozi anayesimama anasema CCM hoyee?" Mtendaji akaniambia alikuwa rafiki yangu akaniita akaninong'oneza, "kijana kaa kimya utapotezwa". Nilishtuka sana
Kiko sehemu gani mheshimiwa. Kwani English medium ni mradi? Si wananchi wanaamua wenyewe TU shule hii iwe English medium kwa wanaoweza kulipa ada. Handeni Kuna wazigua wangapi wanaoweza kulipa ada watoto wao wasome English medium pre and primary school? Shule kama ipo siitakuwa wamejaa wageni TU humo? Nonsense.
Handeni Wana English Medium Pre and Primary School
 
Ni kawaidi, hata kwenye mkoa wetu wa Njombe hakuna mradi hata mmoja.
 
Kiko sehemu gani mheshimiwa. Kwani English medium ni mradi? Si wananchi wanaamua wenyewe TU shule hii iwe English medium kwa wanaoweza kulipa ada. Handeni Kuna wazigua wangapi wanaoweza kulipa ada watoto wao wasome English medium pre and primary school? Shule kama ipo siitakuwa wamejaa wageni TU humo? Nonsense.
Mtanzania mmoja anamuita mtanzania mwingine mgeni katika nchi moja. Ubaguzi kumbe bado upo kwa kiwango kikubwa, jambo la kushukuru Mungu serikali haipo kubagua raia/wananchi wake na itaendelea kuwapa huduma kwa miradi mbalimbali ya maendeleo bila kujali unatokea upande gani wa nchi, dini, kabila au rangi yako.

Ni kawaidi, hata kwenye mkoa wetu wa Njombe hakuna mradi hata mmoja.
Je ni 100% CCM kama Tanga?. Sasa hivi CCM inahangaika zaidi na mikoa ya wasukuma kwa hofu ya kukosa kura, ni uongo?
 
Mtanzania mmoja anamuita mtanzania mwingine mgeni katika nchi moja. Ubaguzi kumbe bado upo kwa kiwango kikubwa, jambo la kushukuru Mungu serikali haipo kubagua raia/wananchi wake na itaendelea kuwapa huduma kwa miradi mbalimbali ya maendeleo bila kujali unatokea upande gani wa nchi, dini, kabila au rangi yako.

View attachment 3218311
Huna maarifa mapana, kila kabila Lina asili yake na nilazima lionje keki ya taifa kwa usawa. Kama akili hiyo huna unawezaje kuchaguliwa mbunge wa jimbo hilo? Purchasing power ya kabila lako lazima ikuzwe ili wamudu kununua huduma zinazowanguuka. Mzanzibar lazima ajue wazanzibar wanapata nn kwenye keki ya taifa.
 
Mimi ni mkaazi wa Tanga(muhamiaji kutoka Ngorongoro). Kuna siku tulikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Kijiji. Mwenyekiti, mtendaji na diwani wakawa wanasema CCM hoyee..! Muda wa maswali ulipofika nikauliza "huu ni mkutano wa hadhara au wa chama?, mbona Kila kiongozi anayesimama anasema CCM hoyee?" Mtendaji akaniambia alikuwa rafiki yangu akaniita akaninong'oneza, "kijana kaa kimya utapotezwa". Nilishtuka sana
Ahaaa, nimekukumbuka! Kumbe yule jamàa pingapinga ndo wewe Restless Hustler ?
 
Hiyo bara bara tu ya Tanga mjini mahandaki yana afadhali kabisaa angalia bara bara ya nne hovyo kabisa, nenda panaitwa sijui mabanda papa mpaka Pangani road yote ile kuna nini pale ? Inatia kinyaa kabisa shida ya Tanga Elimu, Elimu ya kujitambua na elimu dunia ndogo sana umwinyi na kuridhika imetawala kabisa
 
Huna maarifa mapana, kila kabila Lina asili yake na nilazima lionje keki ya taifa kwa usawa. Kama akili hiyo huna unawezaje kuchaguliwa mbunge wa jimbo hilo? Purchasing power ya kabila lako lazima ikuzwe ili wamudu kununua huduma zinazowanguuka. Mzanzibar lazima ajue wazanzibar wanapata nn kwenye keki ya taifa.
Tuna kazi katika safari hii ya maendeleo

Haya nenda Kawa swage ndugu zako walio faulu kidato cha kwanza ili waende shule, wengi wamegoma kwenda shule (kuonja keki ya taifa kama unavyoita mwenye maarifa mapana)

Wanajengewa shule na hawataki kwenda shule
 
Back
Top Bottom