BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wanafunzi 12 wa shule ya Sekondari Handeni iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga wamekamatwa vichakani wakivuta bangi na kucheza kamari muda wa masomo hali iliyopelekea uongozi wa shule hiyo kuwasimamisha masomo kwa muda wa siku 14.
Wanafunzi hao wamekamatwa kufuatia oparesheni maalumu ya kuwasaka wanafunzi watoro katika shule za sekondari Halmashauri ya Mji Handeni ikisimamiwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mussa Mkombati.
Mkombati amesema wanaendelea kuthibiti utoro katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuona watoto wanaripoti shule na kupata elimu.
Baadhi ya wazazi wamepongeza hatua zilizochukuliwa viongozi pamoja na walimu katika kuthibiti utoro huo na kuomba ushirikiano zaidi kutoka kwa walimu.
Jumla ya wanafunzi 214 waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 bado hawajaripo shuleni mpaka sasa.
MWANANCHI