Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Siku Zanzibar ikijitenga kutoka kwenye muungano GDP yake itapanda na kuweza kufanana na WA nchi kama Luxemburg au Liechtenstein.
 
Zanzibar iiombe radhi tanganyika kwa lipi kwani marehemu anaombeka radhi?
Tanganyika si marehemu, tafadhali! Marehemu anaweza kumtawala aliye hai? Si inasemekana Tanganyika inaitawala Zanzibar kimabavu?
 
Mioyo ya Wazanzibar ilishaukataa Muungano siku nyingi. Tuko nao kimwili lakini si kifikra.

Ughaibuni huwa wanajitambulishaje? Mtanzania? Dhubutu!!!

Wanaojiita Watanzania ni Watanganyika. Mzanzibar akiwa ng'ambo hajiiti Mtanzania, bali Mzanzibar!!!
Thubutuuuuuu kuomba radhi kwa lipi.
 
Leo, tumeona ndugu zetu wapalestina walivo jitoa muhanga dhidi ya utawala wa wazayuni. Nyerere alipofanya mapinduzi alitumia mkataba wa utawala wa uingereza dhidi ya Ieland kututawala. Wapalestina waliwerkewa Balfour declaration na waingereza pia. Sisi wazanzibari na ndugu zetu wapalestina hatuna tafauti ila kuwa wenzetu wanatumia nguvu kujitoa kwa mkoloni na sisi tumekuwa matabaka, hatuwezi kujitoa kwa njia nyengine ya amani. Tunategemea kuchoka kwa mtawala. na wenzetu wanategemea kujikomboa. Wenzetu wa Ireland wamejikomboa. wazenji nao waamke na tutafute njia ya kujikomboa. Ukoloni na udhalilishwaji basi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…