Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Muungano ulikuwa 'CIA' project ya kuimeza Zanzibar ndani ya Tanganyika kama njia ya kuua ukomunisti huko Visiwani.
Kati ya Tanganyika na Zanzibar, ipi imeimeza mwenzake?
 
Mkuu, ndivyo ilivyokuwa? Mbona hatukufundishwa hayo mashuleni?

Lakini wewe unayaonaje hayo mapinduzi, yalikuwa Mapinduzi Tukufu kweli au Mauaji Katili?

Nani aliyekuwa katika njia sahihi? Nyerere kumsaidia mpindua Serikali halali au Mwingereza aliyetaka kuirejesha madarakani Serikali iliyopinduliwa?
Ni politics tu zinaendelea. There's no way majeshi ya Tanzania yangeweza kudefend Zanzibar dhidi ya Waingereza.
 
Ni politics tu zinaendelea. There's no way majeshi ya Tanzania yangeweza kudefend Zanzibar dhidi ya Waingereza.
Ninaiunga hoja mkono kwa mantiki hii, kwamba kama ni kweli Jeshi la uingereza liliwagwaya Watanganyika, Uingereza isingekubali kumsaidia Nyerere Jeshi lilipotaka kumpindua mwaka 1964.
 
inasemekana mtoa huu uzi ni mzanzibar kama feitoto
Mkuu! Mkuu! Mkuu! Nimekuita mara tatu! Tafadhali sana usinichonganishe na nchi yangu nzuri Tanganyika.

Tanganyika ni kwetu. Nimezaliwa na kukulia Tanganyika. Wazazi wangu wote, na mababu zangu walizaliwa na kuzikwa Tanganyika.

Nishafika Zanzibar ingawa urojo ulinishinda.

Najua Wazanzibar ni ndugu zangu, lakini hilo hallitanifanya niisaliti nchi yangu nzuri, Tanganyika.

Wazanzibar ni ndugu zetu, lakini wao wana Zanzibar yao na sisi tuna Tanganyika yetu
 
Sawa. Lakini ukweli ni kwamba serikali 3 kiuhalisia ni kuuvunja muungano; itakuwa ni kuthibitisha hatuna nia ya kuungana. Rais wa JMT ataishia kuwa a lame duck president!

Fikiria. Zanzibar hadi leo wanatambua katiba yao ndiyo yenye nguvu juu ya ile ya JMT! Muungano wa kweli unahitaji kukubaliana katiba moja na serikali moja tu. Nje ya hapo tutaendelea kupigiwa porojo za “kero za muungano” zikiambatana na “kamati za usuluhishi” zikitengewa posho za mabilioni ya walipa kodi mazuzu.
Upande wa Zanzibar siku zote na mara zote takwa lao ni Serikali tatu au Angalau zibaki kama zilizopo mbili lakini Serikali moja hawataki hata kusikia habari zake !
 
Mwandishi Dr. Ghasani hakuyashihidia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar bali amehadithiwa kwa fasihi simulizi na mashuhuda wa Mapinduzi Matukufu yale, na kuuageuza fasihi andishi akaandika kitabu chenye urongo
Ukisema mwandishi hakuyashuhudia mapinduzi una maana gani? Kw

amba alikuw hajazaliwa wakati wa mapinduzi au wakati huo hakuwepo Zanzibar? Natarajia hili amelieleza.
Nakushauri mwamini shuhuda unayemsikiliza kwa masikio yako na sio mrongo aliyesimuliwa urongo, akaandika urongo bila kuwa na uhakika mrongo ni nani kati ya aliyemsimulia, au aliyeandika, anaweza kabisa kuwa alisimuliwa ukweli, lakini mwandishi akaandika urongo kwa malengo yake. Ms
Hayo unayonikataza kufanya ndo sasaunafanya wewe. umesema nimsikilze huyo wako anaysimulia ila kumbuka kuwa Dr. Ghasan amesema kuwa alizungumza na wahsika wenyewe na kuna sehemu kanukuu yaliyosemwa na kuna wakati kaparaphrase. Mkuu siku zote hoja lazima ziwe na mashiko vinginevyo hazitokuwa hoja.

Mwandishi Dr. Ghasani hakuyashihidia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar bali amehadithiwa kwa fasihi simulizi na mashuhuda wa Mapinduzi Matukufu yale, na kuuageuza fasihi andishi akaandika kitabu chenye urongo.
 
Kikubwa Sisi sote ni watu wazima. Hakuna kitu kibaya kama dharau. Ifike mahali Katiba ya warioba ipitishwe Tu au kama vipi Zanzibar ijitenge
Binafsi ningekuwa Mzanzibar kwa idadi Ile ya watu ningejitenga Tu ili nifaidi mafanikio mengi na fursa kibao. Zanzibar Wana fursa kupitia nchi za kiarabu lkn pia utalii kutokana na historia. Watakuja na uchumi kubwa Sana na Ajira nyingi saaaana. Wakifungua balozi hata 30 zao huko duniani watakuja mbali saaaana.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Upande wa Zanzibar siku zote na mara zote takwa lao ni Serikali tatu au Angalau zibaki kama zilizopo mbili lakini Serikali moja hawataki hata kusikia habari zake !
Sawa kabisa mkuu. UKWELI ni kwamba Zanzibar hawautaki huu muungano wala hawakuwahi kuutaka tangu awali. Ni kama vile walilaghaiwa au kushurutishwa kijanja na Tanganyika enzi hizo.

Ndio sababu ya wao leo hii hawaoni tabu kujitambulisha kimataifa kama Wazanzibari na kuonyesha dharau za wazi wazi kwa Tanzania bara (Tanganyika) bila kujali “hatari” ya kuvunjika kwa muungano. Kumbuka: “muungano ni kama koti tu; likikubana unalivua”.

Swali kubwa: Tanganyika ina maslahi yapi mazito kiasi cha kuutaka na kuung’ang’ania muungano huu kwa hali na mali au tuseme kisahihi zaidi: by hooks and crooks?
 
Pengine unawanufaisha "wakubwa" wa Tanganyika.
 
Duh 🙄 by hooks and crooks ?! Kazi kweli kweli !
 
Tanganyika inafaidika nini na Zanzibar? kaulize kwenye hizo inasemekana zako
 
Mkuu Mayalla, unaonaje ukaandika na wewe kitabu kitakachoeleza KWELI TUPU za MAPINDUZI NA MUUNGANO?

Nishazisoma bandiko zako kadhaa. Ni wazi kuwa unayafahamu mengi, na umekuwa ukiyawasilisha, wakati mwingine, kimafumbo.

Unaonaje ukiweka kila kitu wazi kwa njia ya kitabu?

Najua wewe ni mtu "mkubwa!" Huogopi.

Mwaka 2016, ulithubutu kumwuliza Amiri Jeshi Mkuu swali ambalo wenzako, pengine wasingethubutu kuliuliza!

Mwaka 2018, ulidiriki kuandika kile unachokiamini ni sahihi bila kujali kuwa kutamkasirisha mkuu wa moja ya mihimili nchini!

Bila shaka, uliyafanya hayo yote kwa maslahi mapana ya Taifa!

Unaonaje ukaandika na kitabu kitakachokuwa na KWELI TUPU, tena bila mafumbo, kuhusu MAPINDUZI NA MUUNGANO?

Ukifanya hivyo, utakuwa umetoa zawadi kubwa sana kwa vizazi vya sasa na vya baadaye!

Tafadhali mkuu, andika kitabu, na usiweke mafumbo! Tafadhali 🙏🙏🙏
Asante, ombi limepokelewa, nalifanyia kitu kinachoitwa objectivity test kama ukweli huu ukijulikana, utasaidia au utasambaratisha? Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
 
Back
Top Bottom