Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Mioyo ya Wazanzibar ilishaukataa Muungano siku nyingi. Tuko nao kimwili lakini si kifikra.

Ughaibuni huwa wanajitambulishaje? Mtanzania? Dhubutu!!!

Wanaojiita Watanzania ni Watanganyika. Mzanzibar akiwa ng'ambo hajiiti Mtanzania, bali Mzanzibar!!!
Muungano uvunjwe haraka
 
Inasemekana pia Marehemu Mzee Karume alisema huu muungano ni kama koti tu likikubana unalivua !!
Inasemekana vile vile, hata Hayati Aboud Jumbe alipojaribu kukurukuka, aliambulia kupokonywa uhuru wake ndani ya nchi huru!
 
Ubovu wa mada yako nzima unauonyesha hapa.

Umetumia "inasemekana", katika sehemu zote, hata haya unayoyashuhudia mwenyewe, kana kwamba nawe huna akili za kuona na kutambua?

Tueleze, wewe leo hii unauonaje Muungano huu, ambao nchi moja iliyoungana na nyingine iliendelea kuwepo, na ile nyingine ikapotea, kama iliyomezwa. Sasa inaonyesha waziwazi nchi iliyobaki bila kumezwa, pamoja na udogo wake inaitawala ile iliyomezwa, na kuondoka!

Swali unalotakiwa kujiuliza kwa hofu kubwa ni hili: je ile nchi iliyomezwa itatapikwa na kurudi kuwepo?

Hilo liinchi lililomezwa likirudi, sidhani kwamba mtaendelea kujibaragaza kama mnavyofanya sasa hivi.
Hivi ni kweli nchi kuubwa na nzuri, Tanganyika, imo tumboni mwa nchi ndoogo inayojiamini, Zanzibar?
 
Inasemekana pia Marehemu Mzee Karume alisema huu muungano ni kama koti tu likikubana unalivua !!
Inasemekana alisema hivyo, na Wazanzibar wanatamani ingekuwa rahisi kulivua hilo "limkoti" kama hayati Karume alivyosema.
 
Tanganyika hatuna la kupoteza muungano ukivunjika ila Zanzibar watapoteza bajeti, nafasi tele za uteuzi, biashara, ajira nyingi, na mali nyingi ikiwemo ardhi wanazomiliki huku bara.
Issue kubwa kwetu ni usalama na ndicho ambacho kinafanya mpaka leo Zenji hatujataka kuiachia

Usalama wetu ni muhimu sana tusipoulinda hiki kisiwa cha amani kinachoitwa Tanzania kitabaki historia

Tukiwaacha wenyewe wajiamulie masuala yao, siku si nyingi vitaanza vikundi vya kigaidi hapo na kwa jinsi ilivyo ngumu kulinda mpaka wa bahari itakuwa ni ngumu kujilinda kuanzia Tanga mpaka Mtwara

Huo upenyo watautumia kuvuruga amani yetu kwa kuleta silaha na kuzua taharuki huku bara kitu ambacho bora kisitokee
 
Zanzibar inafahamika, na Tanzania tunaijua, lakini Tanganyika iko wapi?
 
Hivi ni kweli nchi kuubwa na nzuri, Tanganyika, imo tumboni mwa nchi ndoogo inayojiamini, Zanzibar?
Watu wenye uwezo wa kulijibu swali lako hili ni akina Samia na CCM yake.

Sisi waTanganyika wengine hatuamini hivyo, ndiyo maana wakati umefika sasa tuachane na upuuzi huu wanaofanya CCM.
 
Back
Top Bottom