Baada ya kuuza vikubwa vyote, sasa vya kati vimeanza kuchukuliwa.. Kama tusipogutuka kwenye hili pia tumekwisha. Sasa ni zamu ya shule ya Msingi Ubungo shule ya umma!
Miezi miwili iliyopita kiliuzwa kituo cha mabasi madogo ya abria maarufu kama simu 2000.. Tulipiga kelele za hapa na pale likapita hilo.
Asili ya haya manunuzi ni kuuzwa kwa iliyokuwa stand kuu ya mabasi Ubungo ambayo ilikuja kuhamishiwa Mbezi Luois. Stand hiyo ya zamani sasa panajengwa kituo/soko kubwa la bidhaa za kichina.
Stand ya simu 2000 wameuziwa watu wa DART. Shule haijajulikana vema kauziwa nani. Kuna kila dalili eneo lote la Ubungo lenye huduma za Jamii litamegwa vipande vipande mpaka watalimaliza. TBS ya zamani pengine iko mbioni. Soko la simu 2000 nalo sidhani kama litapona. Mahamaka ya mafisadi je.nknk
Huko tuendako hata wananchi watafurushwa ni swala la muda tu. Baada ya kumaliza Ubungo kituo kinachofuata most likely ni urafiki.. Muda utasema.