Tanganyika/Tanzania iliachwa yatima tangu Ujerumani iliposhindwa vita ya WWII

Tanganyika/Tanzania iliachwa yatima tangu Ujerumani iliposhindwa vita ya WWII

Nyambiza jr

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
1,033
Reaction score
1,841
Habarini wana GreatThinkers nimeona niwaletee hii baada ya kuona na kufuatilia mwenendo wa nchi yetu tangu ipate Uhuru.

Mungu ametubariki nchi nzuri yenye kila aina ya resources na wakoloni kuvutiwa sana na nchi yetu walianza Waarabu kwa kufanya biashara ya utumwa na biashara zao nyingine baada ya hapo walikuja Wamisionari hasa Wajerumani walichukua eneo kubwa sana la nchi yetu na kutujengea miundombinu mbalimbali.

Ilipokuja kutokea Vita ya pili ya Dunia na Ujerumani kushindwa hapo ndipo nchi yetu ilipoenda mrama ilipokabidhiwa kwa Uingereza ambapo watawala hawa wapya walibaki kuishikilia tu hii nchi bila kutengeneza mikakati endelevu.

Mnamo 1961 wazalendo wa nchi yetu waliamua kudai Uhuru rasmi wakiongozwa na Mwl. J. K. Nyerere ambapo tuseme hapo ndipo nchi ilipoanza kujengwa na kiongozi huyu mzalendo kwa kutengeneza mikakati ya yakinifu na mifumo ya kuipeleka nchi mbele na alifanikiwa kwa kiasi chake.

Mwl. J.K.Nyerere alimpasia kijiti Ally Hassan Mwinyi cha kustaajabisha Mweshimiwa huyu alikuja na mfumo wake wa pekee wa kuiendesha nchi kwa kuachana na Viwanda vyetu na kuruhusu bidhaa za nje kuingia nchini "RUKSA".

Baada ya hapo alikuja Mhe. Mkapa ambapo naye alipoona suala la Viwanda limefeli akaamua avibinafsishe na yeye kuja na mfumo wake.

Baada ya hapo alikuja Kikwete nae pia alikuja na mifumo yake.

Magufuli nae alikuja na mifumo yake mipya tena yeye aliamua kurudi hatua kumi nyuma na hakuweza kumaliza kile alichokusudia.


Mpaka hapo utaona ni jinsi gani nchi yetu imepitia katika mikono ya watu tofauti na kila mtu akija na wazo lake binafsi ni sawasawa na mtoto yatima ambae hana msimamizi maalum wa kumuongoza kufukia hatua ya mafanikio.

Je nini kifanyike kuikomboa hii nchi Yatima???
 
Back
Top Bottom