Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi katika makazi ya Mishamo katika Mkoa wa Katavi, yenye vijiji kumi na sita (16)wamelalamikia uongozi wa mkuu wa makazi kuwakosesha uhuru wa kufanya chochote na kujiona bado ni wakimbizi ilhali walishapewa Uraia.
Baadhi ya viongozi wa vijiji hivo wameeleza kuwa hawana uhuru wa kutoka ndani ya makazi bila Kibali maalumu kutoka katika ofisi ya mkuu wa Makazi.
Ili kutoka au kusafiri nje ya makazi lazima wapewe kibali cha kutoka kisichozidi wiki 3na ndani ya huo muda wawe wamesharudi hata kama una mgonjwa amelazwa Hospitali inawalazimu kuomba kibali na hakizidi wiki tatu.
Pia wakazi hao hawaruhusiwi kuhama nje ya makazi yao kwenda kufanya shughuli nje hivyo basi kufanya vijana na baadhi ya watu wazima kutoroka nje ya Mkoa huo na kwenda mikoa mingine kutafuta maisha.
Taasisi za kijamii haziruhusiwi kuingia Na kutoa huduma mbalimbali za kijamii katika Makazi hayo ya Mishamo bila Kibali maalumu toka katika ofisi ya mkuu wa makazi.
Pamoja na Mambo mengine wakazi hao wamekuwa wakilalamika kuwa ijapo walishapewa uraia na kuwa. Watanzania lakini bado hawako huru kama ilivo kwa watanzania wengine.