Tanganyika yetu hiyo yarudi kwa kishindo

Tanganyika yetu hiyo yarudi kwa kishindo

Nyie Watanganyika miaka yote mulikuwa mumelala fofofo sisi Wazanzibari tulikuwa na mpaka leo tunakupiganieni irejeshwe Tanganyika yenu iliyojificha ndani ya Tanzania ikawa wengi wenu munatuona wabaya kwa kusema Tanganyika imekufa. Mpaka leo mzee Warioba kakuamsheni kwenye huo usingizi ndio sasa munaanza kuipenda na kuitaka tena Tanganyika. Wanasiasa kina Nyerere ndio waliokupotezeni. Wazanzibari tuko pamoja na nyie katika kudai nchi yenu Tanganyika. All the best
Asante lakini kumbuka aliyelala ukimwamsha usije lala wewe sasa!!!!!!
 
angalia isifike siku ukasema wale watanganyika na wewe ni wa kanda ya ya ziwa
 
Watanganyika ni wengi kwenye bunge la katiba??? Jina la hovyo kabisa eti Tanganyika!
Usiseme hivyo...tema mate chini....hilo ni Tanga(N'tanga ni samaki mwenye akili sana na hakamatwi kirahisi maana huruka juu kukwepa nyavu za wavuvi. )....Nyika(Nyika ni samaki wa ajabu sana, yeye anatoa 'umeme', ukimshika anapiga 'shoti'.) Kwa maneno mengine Tanga inawakilisha pwani na Nyika inawakilisha pori soma maana ya Neno hili na uzuri wake
 
Nisaidieni hapa kidogo,
Mie mkulima nitafaidikaje na hii kitu?
Nisije kusheherekea halafu kesho mkaanza kutunyang'anya hata
hivi vijishamba vyetu.
 
Hahahaaaaa umetisha sasa Muungano ni akina nani mkuu na sisi watanganyika si tupo?

...mkuu tumetukanwa na kunyanyaswa sana kwenye muungano kana kwamba tanganyka hatuna uwezo bila zanzibar, kwaiyo sisi kwanza muungano na visiwani baadae, wimbo wetu,benki kuu yetu,...
 
...mkuu tumetukanwa na kunyanyaswa sana kwenye muungano kana kwamba tanganyka hatuna uwezo bila zanzibar, kwaiyo sisi kwanza muungano na visiwani baadae, wimbo wetu,benki kuu yetu,...

Mungu ibariiiiikiiii Tanganyikaaaa Wabarikiii viongozi wakeeee ... Duuuuu sipati picha Ngoja Tanganyika yetu irudi bwana
 
Nisaidieni hapa kidogo,
Mie mkulima nitafaidikaje na hii kitu?
Nisije kusheherekea halafu kesho mkaanza kutunyang'anya hata
hivi vijishamba vyetu.

...mnyang'anywe mara ngapi mkuu,mbona wakuu wako kwenye hatua za mwisho za kuchukua ardhi yote nzuri kwa jina la uwekezaji...
 
Back
Top Bottom