Oktoba 7, 2026, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Maji taka Mtaa wa 10, Kata ya Ngamiani - Tanga yanahatarisha usalama wa afya, kero hiyo imedumu kwa zaidi ya wiki moja sasa, licha ya kuwa mamlaka husika zina taarifa, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, hali inayohatarisha afya za Wakazi na Wafanyabiashara wa eneo hilo kwa mlipuko wa magonjwa.”
Hoja ya awali ~ Maji taka Mtaa wa 10, Kata ya Ngamiani - Tanga yanahatarisha usalama wa afya
Baada ya chapisho hilo, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira – Tanga (TangaUWASA) imesema “Tunashukuru kwa taarifa na tunaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza, jitihada za utatuzi wa changamoto hiyo zinaendelea.”
Leo Oktoba 12, 2026, Mmalaka hiyo imetoa taarifa ikieleza kuwa "Blockage imefanyiwa kazi na kwa sasa line inapelekea vizuri maji, tunawashukuru kwa uvumilivu na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza."