Tanzania Railways Corp
JF-Expert Member
- Mar 23, 2018
- 251
- 595
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa Kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) inapenda kuwaalika wafanyabiashara, watoa huduma, wakandarasi, wasafirishaji wa mizigo na wadau wote katika Kongamano la wadau utakaofanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) siku ya jumamosi tarehe 30 January 2021 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
Lengo la Kongamano hili kuzungumzia fursa zinazoambatana na mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) na kuandaa mpango kazi na ushirikishwaji wa Sekta Binafsi ya Tanzania katika mradi huu wa kimkakati. Mkandarasi mkuu wa mradi na wataalamu wengine wengi wataelezea fursa zilizopo na kujadili namna ambavyo Watanzania wajiandae ili kunufaika na fursa hizi.