Tangazo la biashara la Mtanzania limbukeni

Hata ndani ya Bunge letu kuna watu wa jamii toka nje ya mipaka yetu.

nina wasiwasi huyu jamaa haishi tanzania au aliondoka miaka ya 80....kuna wabunge wahindi/waarabu/wasomali
 
Uliyeleta hii thread ninamashaka na macho yako au kuna tatizo first floor
Think positive,be positive life is too beautiful
 

Aliyetengeneza hili tangazo nimempenda, ana akili sana, nadhani ni pro anayejua kazi yake vizuri. Hapo wewe unaona wote ni wazungu kwa sababu ya ushamba wako, macho yangu yananiambia kuna mzungu mmoja tu! Kachukua race mtoto kutoka katika kila race aliyoweza kuipata, Good business Idea. Halafu unaponda wakati naona post yako unachanganya na "kizungu" sijui uonekane umeelimika kuliko mtengeneza tangazo hilo...teh teh!
 

Naungana na jamaa aliyehoji uwezo wako wa kufikiri!
 
nina wasiwasi huyu jamaa haishi tanzania au aliondoka miaka ya 80....kuna wabunge wahindi/waarabu/wasomali
Kwamba nimeondoka Tanzania zamani sana, miaka ya 80, kiasi kwamba race ya Watanzania imebadilika mimi sijui kwa sababu kumekuwa na influx ya Wahindi, Wachina na machotara. How preposterous! You are the most clueless person in the world when it comes to demographic changes kwa kudhani race ya Watanzania imebadilika kwa vile kuna mbunge msomali na mhindi!

Hilo tangazo haliakishi demographics za watoto wa Tanzania, bali linatukuza taswira za watoto wa kijapani na kizungu ambao sio race ya Watanzania, ulimbukeni uliopita maelezo.


Halafu unaponda wakati naona post yako unachanganya na "kizungu" sijui uonekane umeelimika kuliko mtengeneza tangazo hilo...teh teh!
Kwani "kuchanganya kizungu" ndio kuelimika? Huo nao ni ulimbukeni mwingine, suala hapa sio lugha, bali ni kwamba tangazo hili la kilimbukeni limeshindwa kujaribu kuvutia watoto wa Kitanzania katika marketplace ya Tanzania ya watu weusi.

Kwenye tangazo la biashara Tanzania utawekaje picha za wajapani, wazungu na machotara pasipo mbantu hata mmoja? Ulimbukeni wa watu wetu nalo ni janga la taifa kwa sababu kuabudu race za wengine kunakufanya ushindwe kujithamini na kujitafutia maendeleo na heshima duniani.
 
Mkuu duka lako ni lipi pale jirani??!! Ni lile lenye manguo ya kichina ambalo haliuzi nini???!!!hebu acha kuwalisha wanao magimbi na uone kama hawatakuwa na wan'gavu kama hao...acha vivu mkuu
 
wengi mliochangia habari hii mnauwezo finyu wa kufikiri. Mtoa mada anajaribu kuonyesha jinsi gani tunapoteza identity yetu na kutukuza za wenzetu.
Watu wanashindwa kuelewa meseji ya mtoa mada wanabaki wanamshambulia tu na kumtukana kana kwamba kaandika kitu kisichokuwepo.
Kwanini tusiwe proud na utamaduni wetu??
Mwingine anahoji "eti kwanini umeandika lugha ya kiingereza?" utafikiri hajui kuwa kiingereza ni lugha rasmi hapa nchini.
Tunatakiwa kubadilika kwa jinsi tunavyochangia mada...
 

Mkuu ni kweli unachosema...
 
Toa kidhungu kwanza kwenye. uzi wako ndo!!
 

Je, lugha ni sehemu ya utamaduni? Je, Kiingereza ni lugha yetu?
 

Tanzania ina race ngapi?
 

Point yako ni nini hasa, naona unajikanyaga tu, hebu jadili mada uskike! UBAYA WA HIYO PICHA ILIYOWEKWA HAPO NI NINI?
 
Point yako ni nini hasa, naona unajikanyaga tu, hebu jadili mada uskike! UBAYA WA HIYO PICHA ILIYOWEKWA HAPO NI NINI?

It doesn't reflect uhalisia! Duka la nguo za watoto Dar 75% white kids, watoto wa kiafrica waliopo machotara una paint picha gani kwa watoto wetu? Kwamba black is not a class may chotara kidogo......! You people are so ruined...! You dont even know yourselves anymore.
 
hata alienyosha mkono sio mzungu, nadhani asili ya brazil hivi kwa maana hiyo hapo weusi wapo watatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…