Tangazo la biashara la Mtanzania limbukeni

Tangazo la biashara la Mtanzania limbukeni

Hata ndani ya Bunge letu kuna watu wa jamii toka nje ya mipaka yetu.

nina wasiwasi huyu jamaa haishi tanzania au aliondoka miaka ya 80....kuna wabunge wahindi/waarabu/wasomali
 
Uliyeleta hii thread ninamashaka na macho yako au kuna tatizo first floor
Think positive,be positive life is too beautiful
 
vz.jpg

Sijui tatizo ni shule ama ni exposure ama ni kuchukulia mambo kirahisi rahisi.

Kwa mtu prideful of my race, dignity and country hili duka hata lingekuwa na nguo za watoto nzuri kiasi gani siwezi kumpeleka mtoto wangu humu kamwe, maana akiona haya matangazo ataanza na yeye kutukuza wazungu toka mdogo manake subliminal message hapa ni kwamba huwezi kupendeza unless uwe mzungu. Ndo maana wakaona wakitumia picha za vitoto vi model vya kizungu mali itauzika.

Halafu to top it all off, location ya duka lenyewe, another reason why I would never come close to this store. Barabara tumebadilisha jina from a historic and meaningful Bagamoyo road to Mwai Kibaki, of all the people. Nchi za watu wenye raia walio na uelewa na upeo, li-mayor moja la jiji ambalo kesho kutwa linaondoka kwenye cheo haliwezi likaamka asubuhi ghafla limeshauriwa sijui na nani nyumbani kwake huko likaja likawaambia kuanzia leo jina la huu mtaa ni Yoweri Museveni! Watu watachoma mtaa! Tatizo moja kubwa la Watanzania ni kwamba hatujipendi, hatujithamini, hatujijali na hatufikiri.

Aliyetengeneza hili tangazo nimempenda, ana akili sana, nadhani ni pro anayejua kazi yake vizuri. Hapo wewe unaona wote ni wazungu kwa sababu ya ushamba wako, macho yangu yananiambia kuna mzungu mmoja tu! Kachukua race mtoto kutoka katika kila race aliyoweza kuipata, Good business Idea. Halafu unaponda wakati naona post yako unachanganya na "kizungu" sijui uonekane umeelimika kuliko mtengeneza tangazo hilo...teh teh!
 
Hapo kuna vitoto vya Kichina, Kizungu na vichotara.

Tanzania sio nchi ya Wazungu, Wachina na vichotara, ni nchi ya Wabantu, for the preponderant part.

Kutukuza imagery za kichina na kizungu kwenye advertisement ya nchi ya kibantu ni ulimbukeni uliokithiri.

Tanzania kuna races zote?

Absolutely ridiculous.

Tanzania sio nchi ya race ya Kijapani au ya Kizungu!

Huwezi kwenda China au Uholanzi ukakuta wametangaza nguo za watoto wao kwa imagery za watoto wa Kigogo, never! Ever! It's neeever gonna happen. Lakini watu wa the lowest self esteem kama Watanzania tunatukuza fashion presentations za kigeni. Nadhani huwa wanatucheka sana.

Naungana na jamaa aliyehoji uwezo wako wa kufikiri!
BLACK-ALLURE.jpg
 
nina wasiwasi huyu jamaa haishi tanzania au aliondoka miaka ya 80....kuna wabunge wahindi/waarabu/wasomali
Kwamba nimeondoka Tanzania zamani sana, miaka ya 80, kiasi kwamba race ya Watanzania imebadilika mimi sijui kwa sababu kumekuwa na influx ya Wahindi, Wachina na machotara. How preposterous! You are the most clueless person in the world when it comes to demographic changes kwa kudhani race ya Watanzania imebadilika kwa vile kuna mbunge msomali na mhindi!

Hilo tangazo haliakishi demographics za watoto wa Tanzania, bali linatukuza taswira za watoto wa kijapani na kizungu ambao sio race ya Watanzania, ulimbukeni uliopita maelezo.

Halafu unaponda wakati naona post yako unachanganya na "kizungu" sijui uonekane umeelimika kuliko mtengeneza tangazo hilo...teh teh!
Kwani "kuchanganya kizungu" ndio kuelimika? Huo nao ni ulimbukeni mwingine, suala hapa sio lugha, bali ni kwamba tangazo hili la kilimbukeni limeshindwa kujaribu kuvutia watoto wa Kitanzania katika marketplace ya Tanzania ya watu weusi.

Kwenye tangazo la biashara Tanzania utawekaje picha za wajapani, wazungu na machotara pasipo mbantu hata mmoja? Ulimbukeni wa watu wetu nalo ni janga la taifa kwa sababu kuabudu race za wengine kunakufanya ushindwe kujithamini na kujitafutia maendeleo na heshima duniani.
 
Mkuu duka lako ni lipi pale jirani??!! Ni lile lenye manguo ya kichina ambalo haliuzi nini???!!!hebu acha kuwalisha wanao magimbi na uone kama hawatakuwa na wan'gavu kama hao...acha vivu mkuu
 
wengi mliochangia habari hii mnauwezo finyu wa kufikiri. Mtoa mada anajaribu kuonyesha jinsi gani tunapoteza identity yetu na kutukuza za wenzetu.
Watu wanashindwa kuelewa meseji ya mtoa mada wanabaki wanamshambulia tu na kumtukana kana kwamba kaandika kitu kisichokuwepo.
Kwanini tusiwe proud na utamaduni wetu??
Mwingine anahoji "eti kwanini umeandika lugha ya kiingereza?" utafikiri hajui kuwa kiingereza ni lugha rasmi hapa nchini.
Tunatakiwa kubadilika kwa jinsi tunavyochangia mada...
 
vz.jpg

Sijui tatizo ni shule ama ni exposure ama ni kuchukulia mambo kirahisi rahisi.

Kwa mtu prideful of my race, dignity and country hili duka hata lingekuwa na nguo za watoto nzuri kiasi gani siwezi kumpeleka mtoto wangu humu kamwe, maana akiona haya matangazo ataanza na yeye kutukuza wazungu toka mdogo manake subliminal message hapa ni kwamba huwezi kupendeza unless uwe mzungu. Ndo maana wakaona wakitumia picha za vitoto vi model vya kizungu mali itauzika.

Halafu to top it all off, location ya duka lenyewe, another reason why I would never come close to this store. Barabara tumebadilisha jina from a historic and meaningful Bagamoyo road to Mwai Kibaki, of all the people. Nchi za watu wenye raia walio na uelewa na upeo, li-mayor moja la jiji ambalo kesho kutwa linaondoka kwenye cheo haliwezi likaamka asubuhi ghafla limeshauriwa sijui na nani nyumbani kwake huko likaja likawaambia kuanzia leo jina la huu mtaa ni Yoweri Museveni! Watu watachoma mtaa! Tatizo moja kubwa la Watanzania ni kwamba hatujipendi, hatujithamini, hatujijali na hatufikiri.

Mkuu ni kweli unachosema...
 
Toa kidhungu kwanza kwenye. uzi wako ndo!!
 
wengi mliochangia habari hii mnauwezo finyu wa kufikiri. Mtoa mada anajaribu kuonyesha jinsi gani tunapoteza identity yetu na kutukuza za wenzetu.
Watu wanashindwa kuelewa meseji ya mtoa mada wanabaki wanamshambulia tu na kumtukana kana kwamba kaandika kitu kisichokuwepo.
Kwanini tusiwe proud na utamaduni wetu??
Mwingine anahoji "eti kwanini umeandika lugha ya kiingereza?" utafikiri hajui kuwa kiingereza ni lugha rasmi hapa nchini.
Tunatakiwa kubadilika kwa jinsi tunavyochangia mada...

Je, lugha ni sehemu ya utamaduni? Je, Kiingereza ni lugha yetu?
 
wewe kipofu huoni black kids hapo?au kwako black kids mpaka awe mweusi kama mjaluo?unaishi tz gani wewe?wake up and stop ur negativity.......duka ni la race zote coz tanzania kuna race zote na race zote na race zote zimewakilishwa sasa kama wewe huoni race yako hilo ni tatizo lako

Tanzania ina race ngapi?
 
wengi mliochangia habari hii mnauwezo finyu wa kufikiri. Mtoa mada anajaribu kuonyesha jinsi gani tunapoteza identity yetu na kutukuza za wenzetu.
Watu wanashindwa kuelewa meseji ya mtoa mada wanabaki wanamshambulia tu na kumtukana kana kwamba kaandika kitu kisichokuwepo.
Kwanini tusiwe proud na utamaduni wetu??
Mwingine anahoji "eti kwanini umeandika lugha ya kiingereza?" utafikiri hajui kuwa kiingereza ni lugha rasmi hapa nchini.
Tunatakiwa kubadilika kwa jinsi tunavyochangia mada...

Point yako ni nini hasa, naona unajikanyaga tu, hebu jadili mada uskike! UBAYA WA HIYO PICHA ILIYOWEKWA HAPO NI NINI?
 
Point yako ni nini hasa, naona unajikanyaga tu, hebu jadili mada uskike! UBAYA WA HIYO PICHA ILIYOWEKWA HAPO NI NINI?

It doesn't reflect uhalisia! Duka la nguo za watoto Dar 75% white kids, watoto wa kiafrica waliopo machotara una paint picha gani kwa watoto wetu? Kwamba black is not a class may chotara kidogo......! You people are so ruined...! You dont even know yourselves anymore.
 
hata alienyosha mkono sio mzungu, nadhani asili ya brazil hivi kwa maana hiyo hapo weusi wapo watatu
 
Back
Top Bottom