Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Mwalimu yupo darasani anasema, which is talking? Wanafunzi wanaishia kushangaa.
Tangazo hili la haki elimu ni kama linadhalilisha kada ya ualimu. Je ni kweli walimu wengi hawajui Kiingereza? Sasa inakuaje mtu anafika hadi chuo kikuu hajui kimombo? Je kada nyingine nazo vipi kuhusu kujua kiingereza kwa watu wake?
My take:
Tangazo lile lipigwe stop asap!
------
Tangazo hili la haki elimu ni kama linadhalilisha kada ya ualimu. Je ni kweli walimu wengi hawajui Kiingereza? Sasa inakuaje mtu anafika hadi chuo kikuu hajui kimombo? Je kada nyingine nazo vipi kuhusu kujua kiingereza kwa watu wake?
My take:
Tangazo lile lipigwe stop asap!
------
Hili tangazo nimelitafakari kwa muda na nilichoona haliko fair kwa Walimu wetu kwani linawaonesha kuwa hawajui wanachofanya.
Mwalimu: Okay, we are continued from where we stopping yesterday
Mwalimu: Quip quiet
Mwalimu: Which is talking?
(Wanafunzi wanamcheka Mwalimu wao)
With due respect, Hawa watu wa Hakielimu hawakutumia njia nzuri ya kufikisha ujumbe wao kwa Serikali kwa kuwaumbua Walimu wetu kiasi hiki.
Mimi ninawatoto wanasoma English medium schools na wanafundishwa na Walimu hawahawa wa Kitanzania. Na wako vizuri Sana kwenye hiyo lugha ngeni. Tunapoutangazia ulimwengu kuwa tuna Walimu wasiojiweza kwa lugha ya kiingereza kufundisha Ni kuwadharaulisha Walimu wetu na kuwatangazia soko Majirani zetu.
Sipingi kampeni ya ku promote kiswahili kuwa ndio lugha ya kufundishia na kujifunzia, ninachopinga Ni pale tunapo fanya promotion hiyo kwa kuumbua wengine Kama kwamba ndio sababu ya tatizo katika mfumo wetu wa Elimu.
Ieleweke hata huo ufundishaji wa kiswahili ukianza, hautakuwa mrahisi kwa jinsi tunavyodhania. Maandalizi mapana Ni muhimu kwa mfumo mpana na imara wa Elimu ya Nchi hii.
Walimu wetu waheshimiwe na wathaminiwe. Kazi wanayofanya kwa Nchi hii Ni kubwa na katika mazingira magumu. Tusiruhusu kampeni zinazo wadhalilisha kama tangazo hili la Hakielimu.