Tangazo la Kichina lilivyozua mjadala mitandaoni wa chuki na Ubaguzi wa Rangi mwaka 2016

Tangazo la Kichina lilivyozua mjadala mitandaoni wa chuki na Ubaguzi wa Rangi mwaka 2016

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mnamo Mei 2016, kampuni ya vipodozi ya nchini China iitwayo Shanghai Leishang ilirusha tangazo la kidijitali la Sabuni ya kufulia wa Qiaobi, ambalo lilishtua ulimwengu mzima kwa ubaguzi wa wazi wa rangi.

Tangazo hilo lilimwonyesha binti mmoja wa Kichina akimsukumia kwa utani mwanamume mweusi aliyekuwa na madoa ya rangi kwenye nguo zake ndani ya mashine ya kufulia. Baada ya mashine hiyo kuzunguka, alitoka mwanamume mwingine wa Kiasia mwenye ngozi nyeupe na nguo safi, jambo lililomfurahisha sana binti yule

Watu wengi kwenye mitandao walichambua ujumbe uliokuwa nyuma ya tangazo hilo kama ni kuifanya ngozi nyeusi iononekane kama "uchafu" unaohitaji kuoshwa ili ubadilike na ukubalike.

Tangazo hilo lilisambaa kwa kasi ya ajabu duniani kote kupitia mitandao kama YouTube na Facebook, na kuibua hasira kubwa na shutuma nzito kimataifa. Ndani ya siku 5 takribani ilipata watazamaji Milioni 6.5 kwenye Mtandao wa Youtube

Wadau wa habari na watetezi wa haki za binadamu walilaani vikali tangazo hilo kwa kuwadhalilisha watu weusi na kuchochea ubaguzi wa rangi kupitia masoko ya bidhaa za nyumbani.

Baada ya siku kadhaa za shinikizo na kashfa nzito, kampuni hiyo iliondoa rasmi tangazo hilo kwenye mitandao ya China na kutoa taarifa ya kuomba radhi kwa umma na kueleza hawakukusudia udhalilishaji wala ubaguzi wakati tangazo linatengenezwa

Viongozi wa kampuni hiyo walieleza kusikitishwa kwao na taharuki iliyojitokeza, ingawa walijaribu kujitetea kwa kudai kuwa vyombo vya habari vya kimataifa vilikuza jambo hilo kupita kiasi.

Hadi leo, tukio la Qiaobi linasalia kuwa mfano kuonyesha jinsi kauli, picha , video na maneno ya chuki na ubaguzi unavyogusa hisia na kutokubalika katika jamii

1781704175273.png



 
Hiyo Ilikuwa ni institutionalized racism.

Walijua wanachokifanya.
 
Back
Top Bottom